TTCL

EQUITY

Thursday, November 6, 2014

Vyama sita visivyokuwa na uwakilishi bungeni vyatangaza kuungana ili kuweka mgombea mmoja kwenye uchaguzi.

Wakati vyama vya upinzani vikiwa na umoja wao maarufu kama Ukawa na kutangaza kuungana vyama visivyokuwa na uwakilishi bungeni vimetangaza kuungana na  kuweka mgombea mmoja kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa lengo likiwa kupambana na Ukawa na chama cha mapinduzi.

Akitangaza jijini Dar es Salaam uamuzi wa kuungana katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakilishi wa vyama sita visivyokuwa na uwakilishi  ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha UPDP Bw. Fahilm Dovutwa amesema kuwa wameamua kuungana ili kupambana na Ukawa na CCM ambapo vyama vinavyounda umoja huo ni UMD, SAU, UPDP, AFP, Jahazi asilia na Demokrasia makini. Mmoja wa viongozi wa wanaounda vyama sita vinavyounda vyama hivyo  Bw. Rashid Rai ambaye ni wenyekiti wa chama cha wakulima (AFP) Bw. Rashid Rai amesema kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni msingi wa maendeleo hivyo ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi kushiriki katika uchaguzi huo.

No comments:

Post a Comment