TTCL

EQUITY

Monday, May 5, 2014

Maelfu ya watoto njiti hufa hospitalini nchini kwa ukosefu wa vifaa muhimu



Wakati Serikali ikitafuta mwarobaini wa vifo vya mama na mtoto wanapojifungua, imegundulika kuwa kuna idadi kubwa ya watoto wanaozaliwa kabla ya muda wake (njiti), ambao hufariki dunia kila siku katika hospitali mbalimbali nchini kutokana na ukosefu wa huduma ‘muhimu’ katika vituo vya afya.

Taarifa za kuaminika zilizotufikia katika chumba cha habari kutoka kwa mmoja wa madaktari, ambaye hakutaka jina lake litajwe mtandaoni, Mei 2, mwaka huu, amesema hospitali za serikali jijini Dar es Salaam na mikoani, baadhi ya watoto hao hupoteza maisha kutokana na kukosekana kwa mashine maalumu za kuwahifadhia zijulikanazo kama ‘Incubator’.

Kwa mujibu wa takwimu mbalimbali kuhusu tatizo hilo zinaonyesha kuwa, zaidi ya asilimia 75 ya watoto wanaozaliwa kabla ya mda wake ‘njiti’ nchini Tanzania, wangeweza kuokolewa pasipo kuhitaji uangalizi wa kiutaalam zaidi kama vifaa vinavyohitajika vingekuwepo.

Hata hivyo, katika taarifa iliyowahi kutolewa kwa ajili ya siku ya watoto Njiti Ulimwenguni ijulikanayo kwa jina la (Kuzaliwa Mapema Mno) mwaka 2013, inakadiria kuwa watoto 210,000 nchini Tanzania wanazaliwa kabla ya muda kila mwaka kutokana na tatizo hilo.

Zaidi ya theluthi moja ya vifo vya watoto wanaokadiriwa kufikia 40,000 nchini Tanzania, hufa kila mwaka kutokana na matatizo ya kuzaliwa kabla ya kutimiza muda, ambapo mtoto anatakiwa kuzaliwa kwa kawaida akiwa na uzito wa karibu kilo tatu (2.8Kg) kwa wastani na urefu wa sentimeta hamsini, mimba ikiwa imefikia wiki ya 38 hadi 42.

Aidha, Tanzania ni miongoni mwa nchi chache za Afrika ambazo zimethibitishwa kuwa zimefikia lengo la maendeleo ya Milenia namba 4 juu ya uhai wa mtoto, huku matatizo ya watoto kuzaliwa kabla ya muda yakiwa yanashika nafasi ya pili katika kusababisha vifo vya watoto, baada ya homa ya kifua.

Takwimuya Shirika la Afya duniani (WHO) inaonyesha kuwa asilimia 17 ya watoto wachangakatika nchi zinazoendelea wanakabiliwa na uzito pungufu wa kuzaliwa, ikilinganishwana asilimia 13 ya watoto wanaozaliwa nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment