
Mkurugenzi
wa ubunifu na uboreshaji mitaala katika Taasisi ya elimu nchini nchini
Dkt. WILBERFORCE MEENA amesema mitaala ya somo la uraia na maadili
itaanza kutumika mwaka huu.
Mkurugenzi wa ubunifu na uboreshaji mitaala katika Taasisi
ya elimu nchini nchini Dkt. WILBERFORCE MEENA amesema mitaala ya somo
la uraia na maadili itaanza kutumika mwaka huu kwa elimu ya msingi na
sekondari kwa lengo la kuzalisha wataalam watakaoisambaza elimu hiyo
kwa jamii.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya mafunzo kwa viongozi wa
dini nchini Dkt. MEENA amesema elimu hiyo itasaidia kupatikana kwa
wataalam bora wa utatuzi wa migogoro nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Dini mbalimbali nchini
Mchungaji CONON GODDA amesema lengo la semina hiyo ni kuelezana jinsi ya
kukaa pamoja na kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo na kuandaa
wataalamu watakaotoa elimu ya amani katika jamii.
No comments:
Post a Comment