TTCL

EQUITY

Tuesday, March 10, 2015

Wauaji Albino wachinjwe haraka -Mwana FA

Mwanamuziki ambae amekuwa mstari wa mbele kutetea na kupiga vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi nchini Tanzania Mwana FA ambae kwa sasa anatamba na wimbo wake wa Kiboko Yangu amefunguka na kuonyesha hisia zake kali dhidi ya

Mwana FA
watu ambao tayari wamekutwa na hatia ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na kutaka watu hao wanyongwe haraka ili liwe funzo kwa watu wengine wenye tabia hizo au kwa wale ambao wanafikiri kutaka kufanya unyama huo dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi,Mwana Fa amefunguka hayo leo kupitia kurasa wake wa Twitter na Facebook.
Mwana FA anadai kuwa kama nchi ikitekeleza adhabu hiyo kwa haraka na kwa uwazi itasaidia kuifanya jamii iamini kuwa kweli nchi ipo makini na ipo Serious na suala la mauaji na ukatili dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.
"Inachukua muda gani hawa wanaopatwa na hatia ya kudhuru ndugu zetu maalbino kunyongwa? Naona kama wangechinjwa mapema ingesaidia wapuuzi wenzao kujua nchi ipo serious"
Wiki iliyopita watuhumiwa wannne wa mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi walikutwa na hatia na kuhukumiwa kunyongwa ingawa bado mpaka sasa hakuna mtu hata mmoja ambae amekwisha nyongwa,ndipo hali hii ilipoibua maswali kwa msanii huyo kutaka kujua ni muda gani adhabu hii inaweza kutekelezwa ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wanampango wa kufanya ukatili na unyama dhidi ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

No comments:

Post a Comment