Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kushoto) akiteta jambo na
Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil (kulia) na Naibu Katibu
Mkuu, John Mngodo mara baada ya kumpongeza Waziri huyo mpya, nje ya
Ukumbi wa Mikutano Ikulu, jijini Dar es Salaam. Picha na Felix Mwagara,
Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (kushoto)
akimkaribisha Waziri mpya wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga,
ndani ya ofisi ya waziri huyo iliyopo Mtaa wa Ohio, jijini Dar es
Salaam. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga akisaini kitabu cha wageni
kilichopo ndani ya ofisi yake, mara baada ya Waziri huyo mpya kuingia
ndani ya ofisi hiyo baada ya kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha Mawasiliano-MOHA
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mbarak Abdulwakil (wapili
kushoto) akimfafanulia Waziri mpya wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga
(kulia), shughuli mbalimbali zinazofanywa na wizara hiyo. Kushoto ni
Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo. Tukio hilo lilifanyika katika Ukumbi wa
Mikutano wa Wizara hiyo jijini Dar es Salaam, mara baada ya Waziri huyo
kuapishwa Ikulu leo. Picha na Felix Mwagara, Kitengo cha
Mawasiliano-MOHA
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (kulia) akijadiliana na
watendaji wa wizara hiyo kuhusu masuala mbalimbali ya wizara hiyo, mara
baada ya Waziri huyo kuapishwa Ikulu jijini Dar es Salaam leo. Wanne
kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Mbarak Abdulwakil, anayefuata ni
Naibu Katibu Mkuu, John Mngodo, Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza
(CGP), John Minja, Naibu Mkuu wa Jeshi la Polisi (D/IGP), Abdurahman
Kaniki na Kamishina wa Fedha na Utawala wa Idara ya Uhamiaji, Piniel
Mgonja (hayupo pichani). Picha zote na Felix Mwagara, Kitengo cha
Mawasiliano-MOHA
No comments:
Post a Comment