- "Amini nawaambieni enyi Waswahili wachache mnaotawala; mnategemea kweli kuwa mtawaongoza Watanzania kwa lazima wakati wamepoteza matumaini, na mtegemee kuwa watasalia wamekaa kimya kwa amani na utulivu?"
- "Amani ni zao la matumaini, pindi matumaini yatakapotoweka kutakuwa na vurugu katika jamii."
- "Nitashangaa kama hawa Watanzania watakataa kuasi. Kwanini wasiasi?"
- "Wakati wengi wa wananchi wanapopoteza matumaini unajenga volcano. Volcano hii italipuka siku moja. Labda kama watu hawa ni wajinga."
- "Na hakutakuwa na watu wa kizazi hiki na karne hii ambao watatakiwa kujitoa muhanga kwa ajili ya maisha bora katika siku zijazo wakakubali, wakati wanawaona watu wachache wakiendelea kuneemeka machoni pao bila kujali wakati ujao, wakati wao na watoto wao wakiendelea kuishi katika maisha duni na dhalili."
- "Watanzania watakuwa ni wajinga na mataahira, kama watakubali kuendelea kukandamizwa na watu wachache katika nchi yao wenyewe...."
Na ya saba ambayo aliitoa siku nyingi sana;
7. “Siku inakuja ambapo watu watachagua kifo kuliko fedheha na ole wao wale watakoiona siku hiyo! Na ole wao wale watakakaoifanya siku hiyo isiepukike. Natumaini na kusali kuwa siku hiyo kamwe haitofika" - Mwalimu Nyerere (Januari, 1966)
Na nyingine ya nane;
8. “Kwani fursa iko mbele yetu na inategemea kama tuna ujasiri wa kuichukua. Kwani uchaguzi uliopo siyo kati ya kubadilika au kutobadilika; uchaguzi kwa Afrika ni kati ya kujibadilisha au kubadilishwa – kubadilisha maisha yetu wenyewe kwa mwongozo wetu, au kubadilishwa na matokeo ya nguvu zilizo nje ya udhibiti wetu.. .Tunapendelea kushiriki katika kutengeneza hatima yetu sisi wenyewe” –MwalimuNyerere (Januari, 1966)
Nukuu hizi zimo katika kitabu kinachoitwa : Reflections on leadership in Africa: forty years after independence : essays in honour of Mwalimu Julius K. Nyerere, on the occasion of his 75th birthday ' , by Haroub Othman, VUB University Press, 01 Jul 2000.
No comments:
Post a Comment