Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliwataka wahitimu wa
mafunzo ya uongozi mdogo kutumia mafunzo waliyoyapata ili kuleta
mageuzi makubwa ya utendaji katika sehemu zao za kazi.
Balozi
Seif ameeleza hayo leo katika sherehe za ufungaji wa mafunzo ya Jeshi
la Polisi ngazi ya koplo, sajenti na staff sajenti yaliyofanyika katika
viwanja nya Polisi Ziwani mjini Zanzibar.
Amesema
kuyatumia mafunzo hayo vizuri katika utendaji wa kazi itapelekea
kupunguza uhalifu na kurudisha nyuma maendeleo ya wananchi.
“Nategemea
mtabadilika na kuwa watendaji wazuri wanaochukia rushwa, kesi
zitaendeshwa kwa haraka , haki itatendeka katika kutekeleza majukumu na
haki za binaadam zitazingatiwa kwa lengo la kujenga heshima ya Serikali
na kuleta uhusiano wa karibu baina yenu na Wananchi “Alisema Balozi.
Aidha
alilitaka Jeshi la polisi kutopuuza uhalifu mdogo mdogo kwani uhalifu
huo hatimae hupelekea uhalifu mkubwa na kusababisha uvunjifu wa amani
katika nchi.
Nae
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame amewakumbusha wahitimu
hao kuwa wanawajibu mkubwa wa kuwalinda raia na mali zao pamoja na
kulinda sheria za nchi.
Hata
hivyo amewataka kufanya kazi kwa kutumia elimu waliyoipata chuoni kwa
vitendo, kuwaelimisha na kuwaongoza kwa uweledi askari huko vituoni
mwao.
Kwa
upande wake Mwalimu mkuu wa chuo cha Polisi Zanzibar Deusdedit
Kaizilege Nsimeki amesema Jeshi la polisi litaendelea kuwaelimisha na
kuwahamasisha wananchi ili kuwajengea uwezo na uwelewa wa umuhimu wa
utii wa sheria bila ya kushurutishwa.
Mafunzo
ya uongozi mdogo wa vyeo vya Koplo, Sajenti na Staff sajenti
yalifunguliwa rasmi tarehe 16/02/2016. Yakiwa na jumla ya wanafunzi 1532
kati ya hao kozi ya koplo 591, kozi ya Sajenti 706 na kozi ya Staff
sajenti 235.
Kamishna
wa Polisi Zanzibar Hamdani Omar Makame akimkaribisha mgeni rasmini
Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi kufunga mafunzo ya uongozi
mdogo.
Makamu
wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akipokea salamu ya heshima kwa
Maafisa na wahitimu wa mafunzo ya uongozi mdogo katika chuo cha Polisi
Ziwani Zanzibar.
Maafisa na wahitimu wa uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi wakitoa saluti
kwa mgeni rasmini Makamu wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali.
Makamu
wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akikagua kwaride rasmin
aliloandaliwa na Jeshi la Polisi alipofika kufunga mafunzo ya ungozi
mdogo katika chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
Makamu
wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akimvisha cheo mmoja waaskari
waliofanya vizuri zaidi G.944 Makuza Azekiel Shuka kwa niaba ya wenzake
katika sherehe ya kumaliza mafunzo ya uongozi mdogo kwa ngazi ya Koplo,
Sajenti na Stafu Sajenti yaliyofanyika Chuo cha Polisi Ziwani Zanzibar.
Wahitimu wa uongozi mdogo kwa ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti wakiimba wimbo wa maadili wa Jeshi la Polisi.
Baadhi ya walikwa wakifuatilia sherehe hizo.
Wahitimu wakifurahiya kufungwa kwa mafunzo yao.
Makamu
wa pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi akiwahutubia wahitimu wa mafunzo
ya uongozi mdogo wa Jeshi la Polisi katika viwanja vya Jeshi hilo Ziwani
Zanzibar. Picha zote na Makame Mshenga-Habari Maelezo Zanzibar..
Mkuu
wa Chuo cha Polisi Zanzibar SACP Deusdedit Kaizilege Nsimeki akisoma
risala yake katika sherehe ya ufungaji wa mafunzo ya uongozi mdogo kwa
ngazi ya Koplo, Sajenti na Stafu Sajenti iliyofanyika Chuo cha Polisi
Ziwani Zanzibar.
No comments:
Post a Comment