Makontena mengine 11884 pamoja na magari 2019 
yamebainika kuwa yametolewa katika bandari ya Dar es salaam bila kufuata
 taratibu za ulipaji wa kodi na kulikosesha taifa mapato ya zaidi ya 
shilingi bilioni 49 na kuwataka wahusika walipe haraka.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof.Makame Mbarawa
Waziri
 wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa amesema hayo 
jana jijini Dar es salaam na kuongeza kuwa ukwepaji huo wa kodi 
ulifanywa na bandari kavu zinahusika na makontena na bandari kavu 
zinazohusika na uingizaji wa magari huku akiwataka waliolipa wawakilishe
 vielelezo vyao.
Prof. Mbarawa amesema kuwa kutokana na sakata hilo watumishi 7 wa 
mamlaka ya bandari wanaohusika na bandari kavu za makontena na magari 
wamekamatwa na kufikishwa katika vituo vya polisi kwa hatua zaidi za 
kisheria huku wengine nane wakitafutwa.
Desemba 7 mwaka huu waziri mkuu Kasim Majaliwa alitangaza upotevu wa 
makontena 2431 katika bandari kavu nne za Azam, DICD, JEFAG na PMM 
ambapo safari hii bandari kavu hizo nne zimehusika tena na upotevu na 
makontena hayo mengine.
No comments:
Post a Comment