JIFUNZE UJASIRIAMALI: KUTAFUTA SOKO LA BIDHA ZAKO, KUNAHITAJI UBUNIFU
Ishi Maisha ya Kujihoji
Ninaposema "Maisha ya Kujihoji'' nina maana ya maisha ambayo kila mara ninajitathmini kwa dhati, nikijiuliza kama ninafanya
kilicho sahihi kama impasavyo
Binadamu, pamoja na kujijengea nidhamu binafsi mwenendo wangu.
Ninajaribu kuwa mkamilifu na mwaminifu katika tafakari zangu. Na
ninapoona dalili zozote za ubinafsi au woga, ninajiambia, ''Acha
kujifikiria wewe'' au kuwa jasiri kufanya lile unalojua kuwa ni sawa''.
Jinsi ninavyozidi kurudia jambo hili, ninapata ufumbuzi wa kina zaidi wa
moyo wangu kwa namna amboyo inanisaidia kuepuka maamuzi mabaya na
makosa yanayoweza kufanyika.
Sote tunawajua watu waliojiwekea nidhamu
wakati wa ujana na kupata mafanikio makubwa, ila baadaye wakajawa na
majivuno kiasi cha kuwafanya marafiki wa zamani waseme ''mafanikio
yamemharibu''.
Hali yetu ya ubinadamu hutusukuma katika kubweteka na
mafanikio tuliyojipatia. Kwa bahati mbaya, hata tungefanikiwa kwa kiasi
gani katika maendeleo yetu wenyewe, bado tunaweza kupoteza kila
tulichokwishapata kama hatutajitahidi kuwa waaminifu, watu wa kuihoji
mioyo yetu, na wenye kujifunza kila siku.
Watu kama sisi tunaofanya kazi
kwa bidii bila kukata tamaa, tuna uwezekano wa kumaliza kila siku kwa
kukamilisha majukumu tu bila kujichunguza wenyewe. Lakini tukipania
kuufanya utu wetu utukuke, ni lazima tutafakari kwa makini kuhusu ukweli
wa namna tulivyo, na namna ambavyo tungepaswa kuwa bora zaidi. Endapo utashindwa kuishi maisha ya kujihoji mafanikio pekee yanaweza kuwa maanguko.
No comments:
Post a Comment