Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki
(Mb) akiweka saini katika kitabu cha wageni baada ya kuwasili rasmi
katika ofisi yake leo Jumamosi.
Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais- Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda
(aliyesimama) akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na
Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki (wa kwanza kutoka kulia) kuongea na
watendaji wa ofisi yake baada ya kuapishwa kushika wadhifa huo na Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki
(Mb) (kulia) akizungumza na watendaji wa Ofisi ya Rais-Utumishi na
Utawala Bora mara baada kufika ofisini kwake kuanza kazi leo Jumamosi.
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjella Kairuki
(Mb) (wa pili kutoka kushoto) akiwasili ofisini na kulakiwa na watendaji
wa ofisi yake mara baada ya kuapishwa. Kushoto ni Kaimu Katibu Mkuu,
Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon Nzunda.
…………………………………………………………………………….
Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora
Mhe. Angella Kairuki (MB) ameanza kazi rasmi Leo Jumamosi Desemba
12/2015 mara baada ya kuapishwa Ikulu na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli.
Mhe.
Kairuki akiongea na watendaji wa Wizara yake alielekeza masuala ya
kiutumishi ikiwamo kusimamia nidhamu ya kazi ni jambo la msingi hivyo
kutumia daftari la mahudhurio peke yake haitoshi.
“Tutumie
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kubaini Watumishi
wanaoiba muda wa kazi wa Serikali” Mhe. Kairuki alisisitiza na kusema
kazi lazima zitekelezwe kwa kiwango cha juu.
Mhe.
Waziri Kairuki alisema suala la kufanya kazi kwa kushirikiana na
taasisi nyingine za Serikali ni muhimu kwa kuwaelekeza watendaji wa
Wizara yake kushirikiana na Wakala ya Usajili, Ufilisi na Udhamini
(RITA) kubaini taarifa za watumishi wanaofariki ili wafutwe katika
orodha ya malipo.
Mhe.
Waziri Kairuki alisema ushirikiano katika kazi ni jambo la msingi ili
kushauriana katika kutatua changamoto zinazojitokeza katika utekelezaji
wa masuala mbalimbali ya kiutumishi na kuondoa malalamiko.
Awali,
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi na Utawala Bora Bw. Tixon
Nzunda akimkaribisha Mh. Waziri Kairuki kuongea na watendaji wa Wizara
alisema waajiri wote nchini walishaelekezwa kufanya kazi ya kusafisha
takwimu zisizohitaji katika Mfumo Shirikishi wa Taarifa za Kiutumishi na
Mishahara Serikalini (HCMIS).
Bw.
Nzunda alisema Watumishi wote wenye takwimu chafu (takwimu
zisizohitajika) katika mfumo wa HCMIS watafutwa baada ya kukamilika kwa
zoezi hilo ifikapo mwisho wa mwezi Desemba 2015 na endapo kutakua na
mwajiri atakayekua na takwimu chafu atawajibika kwa kushindwa kutekeleza
agizo hilo.
No comments:
Post a Comment