Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini Tanzania
Profesa Makame Mbarawa ameliagiza Shirika la Maji Safi na Maji Taka
Jijini Dar es Salaam (DAWASCO) kuona namna ya kuweka mita za maji ambazo
mteja hatoweza kutumia maji iwapo hajalipia kwanza (Prepaid).
Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini Tanzania Profesa Makame Mbarawa.
Akizungumza
leo Jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya ziara ya kushtukiza
katika shirika hilo, Profesa Mbarawa amesema kwa kuwekwa kwa mita hizo
kutaisaidia kuiongezea serikali mapato na kuwadhibiti wateja wasiolipa
ankara za maji kwa wakati.
Prof Mbarawa ameongeza kuwa mita hizo mpya zitawawezesha Wananchi
kutumia maji kwa kadri kiasi anachotumia ili kuepusha malalamiko ya
kuongezewa bili lakini pia kuepusha utumiaji wa maji bila kulipia.
Profesa Mbarawa pia ameliagiza kampuni ya maji safi na taka DAWASCO
kuhakikisha inaweka miundo mbinu ya kisasa ambayo itawezesha maji taka
kupita bila ya kumwagika ili kuzuia uchafuzi wa mazingira.
No comments:
Post a Comment