Edward Ngoyai Lowassa anatoka katika ya jamii ya wafugaji Kaskazini mwa Tanzania.
Alizaliwa August 26 mwaka 1953 kijijini Ngarashi Wilaya ya Monduli, mkoani Arusha.
Kitaaluma
Lowasa ni msomi , akiwa na shahada kwanza kutoka chuo Kikuu cha Dar es
salaam na shahada ya Uzamili kutoka Chuo Kikuu cha Bath huko Uingereza
(1983-1984).
Uzoefu katika siasa
Edward Lowasa ni mtoto wa tatu wa Mzee Ngoyayi.
Ingawa baba yake alikuwa mfugaji aliwahi pia kufanya kazi kama tarishi katika serikali ya wakoloni.
Alijiunga na chama cha CCM mara tu baada ya kumaliza elimu yake ya chuo kikuu mwaka wa 1977.
Kabla
ya kugombea ubunge , aliwahi kutumikia jeshi la Tanzania na hata
kupigana katika vita kati ya Tanzania na Uganda vilivyopelekea Idd Amin
kuondolewa madarakani.
Baada ya hapo alikuwa mtumishi wa umma kwa
miaka kadhaa kabla kuteuliwa kuwa mbunge kuwajilisha vijana na kujiunga
rasmi na siasa.
Mwaka wa 1990 alijitosa ulingoni kugombea nafasi ya ubunge katika jimbo la uchaguzi la Monduli.
Alifanyikiwa
kwa miaka yote hii Lowassa ameendelea kulishikilia jimbo hilo la
uchaguzi hadi sasa anapolazimika kuliachia ili kuwania Urais.
Hii
si mara yake ya kwanza kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
,kwani mwaka 1995,alikuwa miongoni mwa watangaza nia 15, hata hivyo
nafasi ikachukuliwa na Benjamin William Mkapa.
Hata hivyo tofauti na matarajio ya wafuasi wake,
Mwaka 2005, Lowassa hakuwania nafasi hiyo, badala yake aliunga mkono
rais anayemaliza muda wake Jakaya Kikwete.
Je Lowassa huyu wa sasa amewahi kuwa nani katika nyadhifa alizozipitia kiserikali?
Edward
Ngoyayi Lowassa amewahi, kuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo,
Ardhi na Maendeleo ya Makazi pamoja na nafasi nyinginezo.
Lakini
pia nafasi za juu alizowahi kuzipata ni pamoja na kuwa Waziri Mkuu wa
Jamhuri ya Tanzania kuanzia mwaka 2005 mpaka Febuari 7 mwaka 2008,
alipolazimika kujiuzulu baada ya madai ya kuhusishwa katika kashfa ya
rushwa ya Kampuni ya Richmond, Madai ambayo bwana Lowassa aliyakanusha
hadi sasa.
Katika siasa,Lowassa anafahamika kama mtu wenye
misimamo mikali,kwa kile anachokiamini mwenyewe kama siasa zinazo
ambatana na maamuzi magumu.
Licha ya kuwa mwanachama wa CCM kwa
miaka 38, bwana Lowassa aliwashangaza wanachama wa CCM kwa uamuzi wake
wa kukihama chama hicho.
Hatua iliyochangiwa na yeye kutoridhrishwa na jinsi uteuzi wa wagombea urais wa kilichokuwa chama chake ulivyoendeshwa.
Alijiunga na chama cha kikuu cha upinzani cha CHADEMA.
Hiki ni mojawapo ya vyama vinne vya upinzani vinavyounda umoja uitwao,UKAWA.
Kufuatia
uamuzi wake wa kubadili chama, Edward Lowasa amelazimika pia kubadili
msimamo wake wa kisiasa na kuwa mpinzani wa chama tawala na sera
aliziunga mkono na kuzitumikia awali, jambo ambalo linawatatanisha
wakosoaji wake .
Hii ni mara yake ya pili kujaribu kuingia ikulu.
No comments:
Post a Comment