TTCL

EQUITY

Monday, December 14, 2015

Waandishi watakiwa kuzingatia maadili ya uandishi

Waandishi wa habari nchini Tanzania wamekumbushwa kuzingatia maadili pale wanapoandika habari zinazohusiana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwa kuwa nyingine zimekuwa na athari kwa jamii pamoja na familia husika.
Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika, Bi. Anna Kulaya.
 
Ushauri huo umetolewa jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika Sheria na Maendeleo barani Afrika, Bi. Anna Kulaya, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari juu ya vitendo vya ukatili wa kijinsia na namna waandishi wa habari wanavyoandika habari hizo.
Amesema kuna matukio mengine ya ukatili wa kijinsia yanatisha lakini baadhi ya vyombo vya habari yamekuwa yakiyaripoti jambo ambalo ni kinyume na maadili katika tasnia ya habari.
Bi. Anna amesema kuwa kukutana huko na waandishi wa habari kutachangia kwa kiasi kikubwa kupunguza athari za unyanyasaji wa kijinsia kutokana na taarifa ambazo mara nyingine hazitakiwi kutolewa kwenye vyombo vya habari.

No comments:

Post a Comment