Askari wa Bunge wakiwa
wamebeba jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa
Mara, Leticia Nyerere aliyefariki nchini Marekani alikokuwa akitibiwa
mara baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere
Dar es Salaam jana jioni. Mwili huo leo utaagwa nyumbani kwa Mwalimu
Nyerere Msasani kabla ya kusafirishwa kwenda Butiama mkoani Mara kwa
mazishi yatakayofanyika kesho.
Mwili huo ukiingizwa kwenye gari maalumu katika uwanja huo.
Ndugu jamaa na marafiki wakijadiliana jambo wakati wa kuupokea mwili huo.
Ndugu, jamaa, marafiki na watoto wa marehemu wakisubiri kuupokea mwili wa mpendwa wao.
Mume wa marehemu, Madaraka Nyerere akizungumza na wanahabari baada ya kuupokea mwili huo uwanjani hapo.
Mtoto wa marehemu (kulia), akifarijiwa na mmoja wa ndugu wakati wakienda kupanda gari kabla ya kuondoka uwanjani hapo.


Rais
wa Simba, Evans Aveva akizungumza na wanahabari akiwemo mwanahabari wa
mtandao huu Rabi Hume (kulia) katika eneo la makaburi ya Kisutu jana 18
Januari. ambapo amemuelezea marehemu aliyekuwa mwanachama wa muda mrefu
wa Simba na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini,
Mhandisi Suleiman Said kuwa alikuwa nguzo muhimu.
Rais
wa Simba, Evans Aveva na mbunge wa zamani wa Kinondoni, Idd Azan
wamezungumzia kifo cha aliyekuwa mwanachama wa muda mrefu wa Simba na
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, Mhandisi
Suleiman Said na kumtaja kuwa moja ya nguzo muhimu ndani ya Simba na
taifa ambaye nafasi yake ni ngumu kuzibika.
Akizungumza
na Mo Dewji Blog, Rais wa Simba, Evans Aveva amesema kifo cha Suleiman
kimekuwa cha kushtusha ndani ya Simba na kifo chake kimekuwa ni pigo
kubwa kwa wadau wa soka nchini kwa kupoteza mtu muhimu katika soka la
Tanzania.
Aveva
amesema Suleiman alikuwa akisifika kwa msimamo wake na hivyo kujipatia
heshima kubwa katika soka la Tanzania lakini pia kuwa mtu mwenye mchango
mkubwa katika klabu ya Simba na kwake binafsi amepoteza mwalimu wake
katika uongozi wa soka.
“Kifo
cha Suleiman kimekuja kwa kutushtukiza kwa wana Simba na hata kwa mimi
kama kiongozi wa Simba, alikuwa na mchango mkubwa katika klabu ya Simba
na hata kwa soka la Tanzania kiujumla na pengo lake itakuwa ngumu kuja
kuzibika,
“Suleiman
alikuwa anasifika zaidi kwa msimamo wake ulikuwa hauteteleki na kwangu
binafsi nimepoteza mwalimu na yeye ndiyo aliyenipokea wakati naanza
kuingia katika mambo ya uongozi ndani ya Simba,” alisema Aveva.
Aidha
Aveva aliongeza kuwa tayari klabu ya Simba imeshatoa rambirambi ya
500,000 na uongozi unataraji kuzungumza kuona ni jinsi gani watamuenzi
Suleiman ambaye aliwahi kuwa kiongozi wa Simba.
Nae
mbunge wa zamani wa Kinondoni na mwanachama wa muda mrefu wa Simba, Idd
Azzan amemtaja Suleiman kama kiongozi bora kutokana na kupenda kujenga
umoja baina ya wanasimba na alikuwa na msimamo ambao uliifanya Simba
kuonekana timu bora hata kama mambo hayakuwa sawa.
Alisema
kuwa Suleiman alikuwa mchapakazi na mwenye roho ya ukarimu mambo ambayo
yatamfanya kuwa akimkumbuka kwa wakati wote kutokana na tabia zake hizo
ambazo ziliisaidia Simba na taifa kwa ujumla kwa kipindi ambacho
alikuwa mkurugenzi wa viwanja vya ndege nchini.
“Alikuwa
ni kiongozi ambaye alikuwa akijenga umoja kwa wanasimba na hakukubali
kuwa na makundi na ndani ya klabu na jambo hilo lilikuwa linaisaidia
Simba kupata matokeo mazuri kutokana na mshikamano alioujenga,
“Ni
pigo kwa Simba kupoteza mwanachama wa muda mrefu wa Simba na taifa kwa
kupoteza mchapa kazi aliyekuwa akiwa ni Mkurugenzi wa Viwanja vya Ndege
Tanzania na katika kazi yake alikuwa mchapa kazi sana alikuwa ana
mipango mingi na maeneo mengi ameyasaidia kupata viwanja vya ndege,”
alisema Azzan.
Aliyekuwa
Mbunge wa Jimbo la Kinondoni, Mh. Idd Azzan akisalimiana na baadhi ya
wanachi waliofika kwenye makaburi ya Kisutu katika mazishi hayo.
Mkuu
wa Wilaya ya Iringa, Bwana Richard Kasesela akisalimiana na wananchi
wengine waliofika katika mazishi hayo katika makaburi ya Kisutu.
NaibuWaziri wa Afya Zanzibar, Bwana Mahmoud Thabit Kombo (alievaa kanzu
na miwani) akisalimiana na watu mbalimbali waliofika kwenye mazishi
hayo.
No comments:
Post a Comment