TTCL

EQUITY

Friday, December 4, 2015

Vigogo 8 wafikishwa mahakama ya Kisutu kwa upotevu wa makontena 349 Bandarini DSM.

Vigogo wanane akiwemo mtuhumiwa namba moja aliyekuwa kamishina mkuu wa forodha wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA Tiagi Masamaki wamefikishwa katika mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka mawili ya kula njama ya kudanganya na la kuisababishia hasara serikali ya shilingi bilioni 12.7.

Watuhumiwa hao ni Tiagi Masamaki, Habibu Mponezya, Bulton Mponezya, Eliachi Mrema, Hamisi Omary, Haruni Mpande, Raymond Louis na Ashrafu Yusuph Khan.
 
Akisoma mashitaka hayo mbele ya hakimu mkazi mkuu wa mahakama hiyo Huruma Shaidi wakili wa serikali Christopher Msigwa amesema katika shitaka la kwanza la kula njama ya kudanganya watuhumiwa hao kati ya june mosi mwaka huu na Novemba 17 ndani ya jiji la Dar es Salaam waliidanganya serikali kuwa makontena 329 yaliyokuwa bandari ya nchi kavu iliyopo eneo la Azamu yametolewa baada ya kodi ya serikali kulipwa na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 12.7.
 
Katika shitaka la pili la kuisababishia serikali hasara serikali ya shilingi bilioni 12.7 chini ya sheria ya uhujumu uchumi kati ya june mosi na Novemba 17 mwaka huu jijini Dar es Salaam walishindwa kutimiza majukumu yao inavyotakiwa na kuisababishia hasara ya kiasi hicho cha fedha.
 
Mara baada ya kusomewa mashitaka hayo hakimu Huruma akageukia upande wa mawakili wa washitakiwa kama wana lolote ambapo licha ya wote kuombea wateja wao dhamana mmoja wa wakili alimuomba hakimu kumpa dhamana mmoja wa washitakiwa ambaye ni mwana mama kwa madai kuwa ana mtoto mdogo.
 
Hata hivyo hakimu Huruma katika majibu yake amewaeleza kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza wala kutoa dhamana hadi mahakama kuu, upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na watuhumiwa wamerudishwa rumande hadi Desemba 17 mwaka huu kesi yao itakapotajwa tena.

No comments:

Post a Comment