TTCL

EQUITY

Tuesday, May 17, 2016

Mama, Mtoto Watelekezwa Gesti!


 GESTI 
Recho Steven akiwa na mwanaye akitokwa machozi kwa uchungu alipokuwa akimwelezea mwandishi wetu (hayupo pichani) namna alivyotelekezwa.

GESTI ATELEKEZWA (2)Na Gabriel Ng’osha,
Dar es Salaam: Wanaume katili! Mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Recho Steven, 25, (pichani), mkazi wa Vigwaza mkoani Pwani ametelekezwa gesti akiwa na mtoto na mwanaume ambaye alijifanya msamaria mwema.
Akilisimulia Uwazi mkasa huo akiwa kwenye gesti hiyo, Manzese, Dar (jina linahifadhiwa), Recho alisema kabla ya mkasa huo, alikuwa na maisha ya kawaida ila matatizo yalianza alipoposwa na mwanaume aliyemtaja kwa jina moja la Kimaro.
Alisema aliishi na Kimaro kwa miezi kadhaa ila alipopata ujauzito, mwanaume huyo na wazazi wake walinitenga.
“Nilijitahidi kuvumilia hadi nikajifungulia porini lakini baadaye alinifukuza nyumbani kwao mchana kweupe.
“Niliishi kwa kubangaiza hadi nilipompata dada aliyenihifadhi huko Vigwaza lakini naye aliniambia niondoke kwani mumewe alikuwa anakuja nyumbani.

“Kabla ya kuondoka, kuna vijana walikuja na walinionea huruma kutokana na maneno niliyowaambia, mmoja wao aliniachia shilingi elfu tano.

GESTI ATELEKEZWA (4)“Baadaye nilikutana na mwanaume ambaye anaendesha malori, nikamsimulia kilichonisibu, akaniambia atanisaidia kumpeleka hospitali mwanangu ambaye ni mlemavu wa mguu wa kushoto, nilitakiwa kumpeleka Hospitali ya CCBRT (Msasani, Dar) kwa ajili ya kunyooshwa.
“Huyo mwanaume nilikwenda naye hadi kwake Kilimanjaro kisha akanipangishia gesti lakini baadaye alinitaka kimapenzi, nilipokataa, akakataa kunihudumia, nikamuomba anirudishe Dar, akanirudisha na kuahidi kunisaidia kumpeleka mwanangu CCBRT.

GESTI ATELEKEZWA (3)“Tulipofika Dar, alinipangia gesti hii na kunipa shilingi 25,000 za matumizi akiahidi kurudi lakini hakurejea hadi deni la gesti likawa limefikia shilingi 27,000 (9,000 kwa siku) na sina namna ya kulilipa, mtoto hali yake ni mbaya,” alisema Recho huku akiangua kilio.
Hata hivyo, Uwazi lilimtafuta Kimaro kwa njia ya simu ambaye alikana kumfahamu Recho.
Jitihada za kumpata mwanaume aliyemtelekeza Recho gesti hazikuzaa matunda kufuatia simu yake kutokuwa hewani.
Recho anaomba yeyote aliyeguswa na mkasa wake na ana moyo wa kumsaidia awasiliane naye kwa namba 0678 810 891 au 0657 486 745.

No comments:

Post a Comment