RAIS mstaafu wa awamu ya
nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, akiwa katika picha ya pamoja na watoto
watatu wa marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman, aliyekuwa mkurugenzi
wa Mamlaka ya Viwanja Vya Ndege Nchini, TAA, wakati alipofika nyumbani
kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, jana Januari 19, 2016 kutoa
mkono wa pole. Marehemu Suleiman alifariki Jumatatu Januari 18, 2016
wakati akifanya mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi na tayari
amezikwa. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said).
RAIS mstaafu wa awamu ya nne
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, jana Januari 19, 2016 amehani msiba wa
aliyekuwa Mkurugezi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini,
marehemu Mhandisi Suleiman Said Suleiman.
Dkt. Kikwete aliwasili nyumbani
kwa marehemu Upanga jijini Dar es Salaam, akifuatana na mkewe Mama
Salma Kikwete majira ya saa 10:30, akitokea kijijini kake Msoga mkoani
Pwani.
Baada ya kiwasili, nyumbani kwa
marehemu Rais mstaafu alipokewa na mdogo wa marehemu, Mhandisi, Nasiri
Said Suleiman, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Bw. Laurent
Mwigune, Mkurugenzi wa Sheria na Mawasiliano ya umma, Bw. Ramadhan
Maleta, maafisa wa TAA, na wanafamilia wengine na kwenda moja kwa moja
kuweka saini kitabu cha maombolezo.
Baada ya kufanya mazungumzo kwa
muda, Watoto wawili wa marehemu ambao wanasoma nje ya nchi nao
waliwasili na kupata fursa ya kusalimiana na Rais mstaafu, Dkt. Kikwete.
Watoto hao ni pamoja na mtoto mkubwa wa marehemu, Mohammed Said Suleiman, na mdogo wake Said Suleiman Said.
Baadaye Rais Kikwete alikwenda
kusaliamiana na mama mzazi wa marehemu, mke wa marehemu na wafiwa
wengine na kisha yeye na msafara wake kuondoka majira ya saa 11 jioni.
Mhandisi Suleiman Said Suleima,
alifariki dunia Januari 18, 2016 majira ya asubuhi wakati akifanya
mazoezi ya kuogelea kwenye bahari ya hindi katikati ya Magogoni na
Kigamboni na kuzikwa jioni ya siku hiyo hiyo.
Marehemu ameacha mjane na watoto watatu, Mohammed, Said na Hosam.
Akisaini kitabu cha maombolezo.
JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Bw. Ramadhan Maleta.
JK akimpa pole mtoto wa mwisho wa marehemu, Hosam Suleiman Said Suleiman
JK akimpa pole mtoto mkubwa wa marehemu, Moahmmed Suleiman Said Suleiman.
JK akimsikiliza Mkurugenzi wa Rasilimali Watu Utawala wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini, TAA, Bw.Laurent Mwigune
JK akisalimiana na mdogo wa marehemu, Mhandisi Nasiri Said Suleiman.
JK akimpa pole mama wa marehemu.
Mama Salma Kikwete, akitoka nyumbani kwa marehemu Mhandisi Suleiman Said, baada ya kuhani msiba wake Januari 19, 2016
JK akisalimiana na Mkurugenzi wa Kazi Maalum wa TAA, Mhandisi Thomas Junior Haule.
JK akisalimiana na Meneja Rasilimali Watu na Utawala, Bw. Mohamed R. Ally.
No comments:
Post a Comment