TTCL

EQUITY

Wednesday, January 20, 2016

Jitihada zaidi zinahitajika kukabili Kipindupindu.


Serikali imetoa takwimu kuhusiana na kuanza kwa mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu Agosti 2015 hadi Januari 17 2016 .
Kwa mujibu wa ripoti hiyo jumla ya watu 14,105 wameugua na kati yao 218 wamepoteza maisha nchini na bado ugonjwa huo upo katika mikoa ya Kilimanjaro, Lindi, Arusha, Morogoro,Simiyu,Mwanza,Rukwa na Dar es salaam.
Kipindupindu ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na aina ya bakteria aitwaye Vibrio cholerae, Ugonjwa huu ni wa kuambukizwa kwa njia ya viini vinavyoenezwa kupitia kwa kinyesi kutoka kwa wagonjwa wenye Kipindupindu.


Vile vile sababu kubwa sana ya ugonjwa huu ni pamioja na Mabomba ya kupitisha maji machafu yasiyofunikwa na matanki ya maji ya kunywa yasiyofunikwa huchangia katika kusababisha mkurupuko wa kipindupindu.

Baada ya Rais John Magufuli kuifanya tar 09 Desemba2015 kusheherekea Uhuru kwa kufanya usafi na Serikali kutangaza kila jumamosi ya mwisho wa mwezi kuwa siku ya usafi lakini kama watendaji hawatasimamia matamko yao kwa dhati na kwa kuzingtia nguvu kazi na vifaa kwa ajili ya kufanyia usafi bado ugonjwa huu utasumbua sana.

Ni dhahiri kwamba jitihada zaidi zinahitajika katika miji yetu kukabili ugonjwa huu hasa uzoaji taka, katika miji yetu bado ni wa kusuasua,madampo ya kuhifadhia taka nayo ni kero kila kona, mifereji na mabomba ya maji taka lazima yatazamwe kwa jicho jingine kwani katika maeneo mengi hasa ya jiji la Dar es salaam chemba nyingi zinavujia barabarani ,usafi wa mazingira ni vyema uwe ajenda ya kila mwananchi.

No comments:

Post a Comment