TTCL

EQUITY

Friday, December 4, 2015

Watendaji watakiwa kuacha kusingizia wanasiasa

Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadick
Hayo yamesemwa leo na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Said Meck Sadick, wakati akipokea vifaa vya usafi na dawa za kuzuia magonjwa ya kuambukiza hususani Kipindupindu vyenye thamani ya Milion 15.

Amesema watendaji wengi wameshindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kubebana na watumishi wao na kushindwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuwasingizia wanasiasa wanawaingilia katika utekelezaji wa majukumu yao.

Meck Sadiki amewataka watendaji hao kutokubali kuingiliwa katika majukumu yao na wasimamie sheria ya kazi zao zinavyowataka na kuacha kuwalea watumishi wazembe.

Kwa upande wao wadau wa maendeleo nchini wameiomba serikali kuhakikisha inasimamia vitendea kazi vinavyotolewa na wahisani.

No comments:

Post a Comment