TTCL

EQUITY

Thursday, November 12, 2015

Benki ya Equity yapata faida ya bilioni 5/-

BENK ya Equity imeweza kupata faida ya Sh bilioni 5.03 katika kipindi cha mwaka unaoishia Septemba 2015 ikilinganishwa na kiasi cha Sh bilioni 1.52 zilizopatikana mwaka uliopita.

Kwa upande wa kampuni tanzu ya Equity imeweza kupata faida ya Sh bilioni 256 katika kipindi kinachoishia mwezi Septemba 2015 ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na Sh bilioni 224 iliyopatikana mwaka jana.

Akizungumza na wanahisa kuhusu taarifa ya hesabu za robo ya tatu ya mwaka, Ofisa Mtendaji wa kampuni tanzu ya Equity Dk James Mwangi aliwaambia mkakati ya uboreshaji hii imewezesha Huduma za kibenki kwenye kanda kukua kwa kasi kubwa.

Alisema pia uwekezaji mkubwa katika njia mpya za uwakala na huduma ya simu mtandao, mafanikio yaliyopatikana katika upanuzi katika nchi za ukanda wa Afrika Mashariki imechangia kwa kiasi kikubwa faida iliyopatikana katika robo ya tatu ya mwaka huu.

Pia faida kabla ya kodi imeongezeka kwa asilimia 14 hadi kufikia kiasi cha Sh bilioni 362 ikilinganishwa na Sh bilioni 318 iliyopatikana katika kipindi cha mwaka jana.

Mafanikio haya makubwa ambayo kampuni tanzu ya Equity imeyapata yametokana na mikakati mahsusi na ubunifu katika kuweka mazingira rahisi ya upatikanaji wa Huduma za kibenki na kuwafanya wateja kupata huduma hizo kwa urahisi na kwa wakati.

No comments:

Post a Comment