TTCL

EQUITY

Wednesday, March 4, 2015

Mafuriko Janga jingine Nchini Tanzania

Mafuriko mabaya kaskazini magharibi mwa Tanzania inasadikiwa kuua zaidi ya watu 42 na wengine 80 kujeruhiwa.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa mvua kubwa na upepo mkali ziliharibu nyumba na kufunga barabara karibu na mji wa Shinyanga na hivyo kupelekea kuzuia kwa oparesheni za kuwanusuru wahanga hao wa mafuriko.

Kamanda wa polisi Mkoa wa shinyanga Justus Kamugisha akiongea na Blogger wetu kwa njia ya simu alisema kuwa mamia ya watu wameachwa bila makao huku zaidi ya watu 80 wakijeruhiwa huku mimea ikiharibiwa vibaya, na mifugo kufa maji.

Haya ni baadhi tu ya mabonge ya barafu yaliyokuwa yakidondoka kama mvua
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, na kusema waliokufa wengi ni watoto ambao walisombwa na maji baada ya maji kujaa ndani ya nyumba zao na kwamba majeruhi wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama. 


Kamanda Kamugisha amesema watu 35 wamekufa eneo la tukio na wengine watatu wamekufa walipofikishwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama na kwamba idadi hiyo inaweza kuongezeka kutokana na majeruhi wengine kuwa na hali mbaya.

Amesema majina ya waliokufa kwa sasa bado hayajatambulika na kwamba kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa wa shinyanga inakaa jioni hii ili kutathimini maafa hayo pamoja na kujua ni msaada gani unahitajika kwa wahanga hao.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi ya wilaya ya Kahama, ambaye ni mkuu wa wilaya hiyo Benson Mpesya akizungumza kwa njia ya simu naye amesema kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya itakaa kabla ya kamati ya mkoa ili kupata taarifa zitakazoisaidia serikali kuanza kutoa misaada.

Akiwa eneo la tukio Mpesya ametoa agizo kwa uongozi Redcross na jeshi la Scauti kuhakikisha wanasaidia katika familia zilizokutwa na maafa hayo wakati serikali ikisubiri kukamilika kwa zoezi la sense ya wahanga hao aliloagiza kufanywa na viongozi wa eneo hilo.

No comments:

Post a Comment