TTCL

EQUITY

Wednesday, April 20, 2016

Uliofanywa na Wilson Kabwe, Mwanza

kabwe 
 Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Wilson Kabwe.

ALIYEKUWA mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje aliwahi kumtuhumu aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji hilo, Wilson Kabwe aliyesimamishwa kazi jana na Rais John Pombe Magufuli.
Wenje alitoa tuhuma hizo bungeni kwenye Bunge la 10, Mkutano wa 18, Kikao cha 7 alipoanika namna ambavyo Wilson Kabwe alishiriki katika usifadi wa Mradi wa Ujenzi wa Kliniki jijini humo huku akitoa maelezo kuwa, ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kuhusu Special Audit ya mwaka wa fedha 2010/2011 ilipendekeza Kabwe achukuliwe hatua jambo ambalo serikali halikuifanya na badala yake akahamishiwa Dar es Salaam.

Ezekiel-Wenje-620x308Aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana jijini Mwanza, Ezekiel Wenje.
 
 
Rais John Pombe Magufuli, jana alimsimamisha kazi Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Bw. Wilson Kabwe kutokana na ufisadi katika utekelezwaji wa mikataba mitatu, inayohusu maeneo ya ukusanyaji mapato ya Stendi Kuu ya Mabasi Yaendayo Mikoani ya Ubungo na kodi ya uegeshaji magari katikati ya jiji na  kuisababishia  serikali  hasara  ya  pesa zaidi ya bilioni 3.
Rais Magufuli amechukua uamuzi huo mchana huu wakati wa uzinduzi wa daraja la Kigamboni, ambapo kabla ya Rais kuhutubia, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda alitoa hotuba fupi ya maswala kadhaa ya Mkoa wa Dar es Salaam  ikiwemo  ripoti ya tume aliyounda  kuchunguza utekelezwaji wa mikataba hiyo.
Kabla ya kuhamishiwa jijini Dar es Salaam, Kabwe alikuwa ni Mkurugenzi wa Jiji la Mwanza ambaye alihamishiwa Mwanza akitokea Mbeya baada ya kutuhumiwa kwa  ufisadi wa mabilioni kadhaa jijini humo.

No comments:

Post a Comment