TTCL

EQUITY

Thursday, April 2, 2015

MELI YA URUSI YAZAMA

Meli ya uvuvi ya Urusi iliyozama kwa dakika kumi na tano tu

Boti ya uvuvi ya Urusi imezama katika visiwa vya Kamchatka , ikiwa na mabaharia wapatao hamsini na wanne ambao inadhaniwa kuwa wamekufa maji wote.
Watu wapatao sitini na watatu wameopolewa ambao nao walikuwa ndani ya boti hiyo ya uvuvi,wengine wamekumbwa na homa ya mapafu na wengine kumi na watano wameripotiwa kuwa hawaonekani.
Taarifa za awali zinasema kwamba kabla meli hiyo ya uvuvi haijazama ilikuwa na watu wapatao miamoja na thelathini na mbili ,uchambuzi unaeleza kuwa sabini na nane kati yao ni raia wa Urusi na arobaini na wawili ni raia wa Myanmar. Wengi wao walikuwa wanatokea maeneo ya Vanuatu, Latvia na Ukraine na nahodha ni miongoni mwa waliopoteza maisha.
Kikosi cha uopoaji kinaendelea na kazi ya oukozi ambapo mpaka sasa wanatafuta abiria hao waliopotea wapatao kumi na watano .
Nahodha wa kikosi cha uongozi ambaye ni miongoni mwa mabaharia wa kikosi cha uopoaji ishirini na sita anasema kwamba pengine chanzo cha ajali hiyo ni hali mbaya ya hewa, na wakati meli hiyo ilipokuwa ikizama ,kulikuwa na barafu,upepo mkali, mawimbi yenye urefu wa futi kumi. Na maji ya bahari yalikuwa karibu yanaganda kwa nyuzi joto 32 .
Inaelezwa kwamba manusura wa ajali hiyo walikuwa wanauwezo wa kudumu katika maji hayo kwa dakika ishirini tu,ingawa mpaka sasa chanzo cha ajali hiyo ni cha kukisia tu.
Maji yalifurika kwenye chumba cha ingini ya meli hiyo na kuanza kuzama ndani ya dakika kumi na tano kimesema kitengo cha dharula cha Urusi,na kusema kwamba pengine meli hiyo iligonga eneo la karibu na chumba cha ingini na kuwa sababu ya ajali hiyo.
Sergei Khabarov amesmea kwamba kiwango cha abiria na mizingo katika meli za wavuvi lazima kizingatiwe na kisizidi uwezo wa vyombo hivyo.

No comments:

Post a Comment