TTCL

EQUITY

Friday, March 27, 2015

Tibaijuka mambo magumu Muleba


MBUNGE wa Muleba Kusini, Prof. Anna Tibaijuka (CCM), ameingia kwenye mgogoro wa ardhi na wapiga kura wake, wakitaka Halmashauri ya Wilaya ya Muleba ipime upya eneo analomiliki na kuligawa.

Hali hiyo inakuja wakati ambapo Prof. Tibaijuka akihaha ‘kujitakasa’ jimboni baada ya kukumbwa na kashfa ya kupokea mgawo wa fedha za Escrow sh. bilioni 1.6 kutoka kwa James Rugemalira.

Kwa mujibu wa wapiga kura wake, tarehe 12 Machi 2015, wanavijiji viwili vya Kimwani na Kyamyorwa Kata ya Kasharunga zaidi ya 300 walifanya mikutano ya hadhara na kuazimia kuwa uongozi wao ufike halmashauri.

“Wananchi walitaka uongozi uombe kuletewa wataalam, waje kupima na kubaini, ni ekari ngapi anazo zimiliki Prof.Tibaijuka. Hatua hii ni baada ya kupewa taarifa na Diwani wa Kata ya Kasharunga (Khalid) kuwa halmashauri ya wilaya Muleba inazitambua ekari 1098.

“Pamoja na taari ya halmashauri, eneo analomiliki ni zaidi ya 4000 kama wananchi wanavyoamini sasa. Malalamiko hayo yamepelekwa kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi kwa muhtasari na Waziri Mkuu kwa msaada zaidi,”wanasema wapiga kura wake.

Taarifa zinaeleza kuwa Prof.Tibaijuka baada ya kupata taarifa hiyo, Jumapili tarehe 22 mwaka huu, amelazimika kwenda Kyamyorwa kufanya mkutano ili kuwalainisha wananchi wake.

Wamesema akiwa Kyamyorwa katika mkutano wa hadhara, Prof. Tibaijuka alikiri kumiliki ekari 1500 licha ya halmashauri ya Muleba kuzitambua ekari 1098.

Kumekuwa na mgogoro mkubwa baina ya wananchi jimboni Muleba Kusini na mbunge wao, wakidai kwamba alishirikiana na halmashauri ya wilaya kuwapora ardhi yao.

No comments:

Post a Comment