TTCL

EQUITY

Sunday, December 7, 2014

Hekima 17 za Nelson Mandela Zinazofaa Kusomwa na Kila Mmoja

Nelson Rolihlahla Mandela was the first democratically elected president of South Africa. Photo released by South Africa The Good News under Creative Commons (CC BY 2.0).
Hayati Baba, (simba wa Afrika)
Nelson Mandela alikuwa rais
wa kwanza wa Afrika Kusini
aliyechaguliwa kidemokrasia
.
Nelson Mandela, rais wa kwanza wa Afrika Kusini kuchaguliwa kidemokrasia na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, amefariki Desemba 5, 2013 akiwa na umri wa miaka 95. Mandela alitumikia kifungo kwa miaka 27 kwa sababu ya mapambano yake dhidi ya mfumo wa kibaguzi wa Afrika Kusini unaofahamika kama  Ukaburu. Aliachiwa huru kutoka gerezani mwaka 1990, na kuwa rais miaka minne baadae, na kuachia madaraka baada ya kutumikia kwa kipindi kimoja tu, kitendo adimu kufanywa na wenye madaraka barani Afrika.

Akiwa mtu anayependwa duniani kote, Mandela alkuwa na namna ya mvuto katika maneno yake. Moja ya nukuu zake inatoka katika hotuba yake ya kijeuri aliyoitoa mahakamani wakati wa Kesi maarufu ya Uhaini ya Rivonia mwaka 1964, ambapoalisema: 
Nimepigana dhidi ya mfumo wa utawala unaowapendelea makaburu, na nimepigana dhidi ya mfumo wa utawala unaowapendela weusi. Nimekuwa na ndoto ya jamii ya kidemokrasia na huru ambayo watu wote wanaishi pamoja kwa mshikamano na fursa sawa. Ni ndoto ambayo nataraji kuiishi na kuitimiza. Lakini, kama itahitajika, hiyo ni ndoto ambayo nimejiandaa kupoteza maisha yangu kwa ajili yake.
Ukiacha hotuba hiyo ya kesi yake ya Rivonia, Mandela anaacha nyuma yake nukuu nyingi za kukumbukwa zenye busara alizozitoa katika kipindi chake chote cha uhai wake. Pamoja na kutuacha, anaendelea kuzungumza na ulimwengu kupitia watumiaji wa twita, ambao waliitikia habari za kifo chake kwa kusambaza maneno yake.

Kuhusu Chuki:
Chuki hufunga akili. Inazuia ubunifu wowote wa mbinu. Viongozi hawana nafasi ya kuchukia
Kama wanaweza kujifunza kuchukia, basi wanaweza kufundishwa kupenda, kwa sababu kwa kawaida ni asili yake upendo kuja kwa moyo wa mwanadamu kuliko kinyume chake
Hakuna aliyezaliwa awe na chuki…Nelson Mandela
Kuhusu Msamaha:
“Watu wenye ujasiri hawaogopi kusamehe kwa ajili ya amani”
Utafanikiwa vingi katika dunia hii kupitia matendo ya rehema kuliko kwa matendo ya kuadhibu watu
Kuhusu Michezo:
Michezo inaweza kuamsha matumaini pale ambapo awali palitawaliwa na kukata tamaa
Kuhusu Uongozi:
“Ongoza kutokea nyuma -na wafanye wengine waamini wao ndio wako mbele.”
Kuhusu Ubaguzi wa Rangi:
“Ninapinga ubaguzi wa rangi kwa sababu ninauchukulia kuwa jambo la kipuuzi, iwe linatoka kwa mtu mweusi au mweupe.”
Kuhusu Kuwa na Malengo Mahususi:
“Mara zote huonekana haliwezekani mpaka lifanikiwe.”
Mtu mwenye akili si yule anayejisikia kuogopa, bali yule aushindaye woga. – Nelson Mandela, katika kitabu chake cha Long Walk To Freedom, 1994
“Heshima ni kwa wale wasioupa mgongo ukweli, hata pale mabo yanapoonekana kufunikwa na giza na kutokufurahisha” -Nelson Mandela
Kuhusu Uhuru:
“Kwa sababu kuwa huru si tu kutupa minyororo, bali kuishi katika namna inayoheshimu na kukuza uhuru wa wengine.”
Kuhusu Elimu:
“Elimu ni silaha yenye nguvu kuliko zote unayoweza kuitumia kubadilisha dunia.” -Nelson Mandela Pumzika kwa Amani
Kuhusu Kufungwa:
“Inasemekana kuwa hakuna anayelijua taifa hadi awe amewahi kuwa ndani ya jela.”
Kuhusu Wajibu:
“Mtu anapofanya kile anachokiona kuwa wajibu wake kwa watu wake na nchi yake, mtu huyo anaweza kupumzika kwa amani” – Nelson Mandela