TTCL

EQUITY

Saturday, December 6, 2014

Mtoto afa kwa kunyongwa na baba wa kambo Morogoro

Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja mkazi wa kijiji cha Kindo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amefariki dunia baada ya kunyongwa na baba yake wa kambo kufuatia migogoro ya kifamilia kati yake na mkewe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro Leonard Paul
Mtoto mwenye umri wa mwaka mmoja mkazi wa kijiji cha Kindo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro amefariki dunia baada ya kunyongwa na baba yake wa kambo kufuatia migogoro ya kifamilia kati yake na mkewe.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul amesema mtoto Abdallah Hamis amenyongwa na baba yake wa kambo Zamili Shabani (27) muda mfupi baada ya mama wa mtoto kwenda dukani kununua mahitaji na aliporejea aliingia chumbani kumwamsha mtoto ndipo akagundua kuwa mtoto amekufa ambapo mtuhumiwa kwa wasiwasi alianza kukimbia na mama huyo alipiga kelele ya kuomba msaada kwa majirani hadi alipokamatwa.
Katika hatua nyingine jeshi la polisi mkoa wa Morogoro linamshikilia mtuhumiwa mmoja Abadalla Kifungo (40) mkazi wa Malola wilaya ya Ulanga mkoani Morogoro kwa tuhuma za kukutwa na silaha aina ya Shortgun na risasi mbili ambapo inasadikiwa kuwa alikuwa akijihusisha na matukio ya ujangili ambapo watuhumiwa hao wa matukio mawili tofauti watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka.

No comments:

Post a Comment