TTCL

EQUITY

Sunday, December 8, 2013

BAADA YA KIPIGO CHA NEWCASTLE: SHABIKI WA MAN UNITED AJIUA KWA KUJIRUSHA KUTOKA GHOROFA YA SABA

 
 
Kijana mmoja anayeaminika kuwa shabiki wa Manchester United Football Club amejiua, jijini Nairobi baada ya timu yake kufungwa 1-0 to Newcastle.
Polisi wamesema kwamba John Jimmy Macharia, 23, alijirusha kutoka ghorofa ya 7 baada ya kujua timu yake imepoteza mchezo wake mechi iliyochezwa juzi jioni. Kwa mujibu wa mkuu wa polisi jiji la Nairobi Benson Kibue, Macharia aliwaambia rafiki zake hawezi kuendelea kuangalia timu yake ikifungwa kila siku kabla ya kuruka ghorofani. “Mashahidi wote waliokuwepo wakati wa tukio bado wapo mikononi mwa polisi wanahojiwa,” alisema. Kibue aliwashauri vijana wa jiji la Nairobi kufahamu English Premier League ni mchezo tu kama ilivyo michezo mingine na hivyo waache kuchukua hatua za namna hii kisa michezo. Hii si mara ya kwanza kwa kijana kupoteza maisha kwa ajili ya michezo inayochezwa  England,” alisema Kibue.

No comments:

Post a Comment