Kashfa za wabunge hao wa CCM zinatokana na hatua yao ya kujiingiza kwenye mahusiano ya kimapenzi kwa nguvu na vijana wadogo.
Rosesweeter
ambaye ana umri wa miaka 60, yuko katika kashfa ya kufunga ndoa na
kinda wa miaka 26, Michael Christian, wakati Profesa Kapuya anahaha
kujinasua na kashfa inayomzingira ya kumbaka binti wa miaka 16, ambaye
sasa anatishia kumuua baada ya kumwaga mtama hadharani.
Ukija
kwenye kashfa ya Rosesweeter kufunga ndoa na kijana wa miaka 26 sio
kosa kisheria, lakini wadadisi wa mambo wanasema kimaadili ndoa hiyo
haikupaswa kufungwa kutokana na umri wa bibi harusi kuwa mkubwa kiasi
kwamba hana uwezo tena wa kuzaa wakati bwana harusi ndiyo kwanza kijana
wa miaka 26 tu.
Wakati
Profesa Kapuya anadaiwa kumbaka msichana huyo mwaka 2011, Rosesweeter
naye alifunga ndoa na kijana huyo mwaka huo huo, Septemba Mosi.
Kabla
ya wawili hao kuamua kufunga ndoa, mbunge huyo kutoka mkoani Rukwa,
mwenye makazi yake Bagamoyo mkoani Pwani, alikuwa akimtumia Michael
kwenye shughuli mbalimbali na muda wote alikuwa akiishi nyumbani kwake.
Inaelezwa
kuwa mbunge huyo ambaye ana familia ya watoto wawili ambao kiumri
wanalingana na Michael, alianza uhusiano wa kimapenzi na kijana huyo kwa
siri kubwa na baadaye alifanikiwa kumshawishi wafunge ndoa huku
akimuahidi kumpa huduma mbalimbali anazotaka.
Hata
hivyo, kashfa ya Rosesweeter kwa sasa imeongezeka baada ya kuamua
kuzuia vyeti vya shule vya kijana huyo baada ya kufunguka macho na
kuamua kuachana na ndoa hiyo ambayo kwa vigezo vyote ni batili.
Wakati
kijana huyo ameamua kuvunja ndoa hiyo kwa kile alichoeleza kukosa
uhuru, manyanyaso na mambo mengine, mbunge huyo anasisitiza kuwa ndoa
hiyo bado halali kwani haijavunjwa kisheria na kuongeza kuwa kinda huyo
bado ni mume wake.
Mbunge
huyo bila kumung’unya maneno anakiri kufunga ndoa na kinda huyo na
kuitangazia jamii kuwa kijana ndiye aliyemdanganya na kumtaka wafunge
ndoa hiyo ambayo hadi leo imebaki kuwa gumzo nchini.
Hata
hivyo, ndoa anayosisitiza mbunge huyo kuwa ni halali, inaelezwa kuwa ni
batili kutokana na ukweli kwamba imefungwa bila kuzingatia vigezo kwani
haijatangazwa mara tatu kama sheria ilivyotaka, imefungwa kwa siri bila
wasimamizi wala mashuhuda katika Kanisa la Mikocheni B Assemblies Of
God Mlima wa Moto linaloongozwa na Mchungaji Getruda Rwakatare.
Tayari
wanaharakati na baadhi ya viongozi wa dini wameandika barua kwa Waziri
wa Mambo ya Ndani kutaka aingilie kati kumsaidia Michael apate vyeti
vyake vya shule, vinavyoendelea kushikiliwa na mbunge huyo na
kusisitiza kwamba hawezi kuvitoa kwani bado kijana huyo ni mumewe.
Kashfa ya Kapuya
Kashfa ya Profesa Kapuya ya kudaiwa kumbaka msichana wa miaka 16, ni aibu kwa mbunge huyo ambaye amepata kuwa waziri.
Mbunge
huyo maarufu nchini, anadaiwa kumbaka binti hiyo kwenye hoteli moja ya
kitalii iliyoko jijini Dar es Salaam mwaka 2011, na kurudia tena kitendo
hicho ndani ya ofisi yake katika jengo la Biashara Complex lililoko
Mwananyamala Juni 3, 2012 alipoitwa kwenda kuchukua ada kwa mara ya
pili.
Wakati
Serikali inakusudia kufungua mashitaka mawili ya kubaka na kutishia
kuua dhidi ya Profesa Kapuya, waziri huyo wa zamani bila woga ameendelea
kutuma ujumbe mfupi kupitia simu yake ya mkononi kwa binti huyo na
kusisitiza kuwa lazima amuue.
Profesa
Kapuya amekuwa akitumia simu yake kuhamisha fedha kwenda kwa binti huyo
ambaye hivi karibuni katika baadhi ya vyombo vya habari alikana
kumfahamu na hajawahi kukutana naye.
Amekuwa
akihamisha fedha kutoka kwenye simu yake namba 0784993930 iliyosajiliwa
kwa jina lake kwenda kwa namba inayomilikiwa na binti huyo.
Tayari serikali kupitia Jeshi la Polisi, imesema inakusudia kufungua mashitaka mawili dhidi ya mbunge huyo.
Mashitaka yanayotajwa kumkabili Kapuya ni ya ubakaji na kutishia kuua.
Kamishna
wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, aliliambia
gazeti hili juzi kuwa jeshi lake halitakuwa na sababu ya kumuacha mbunge
huyo aendelee kutamba mitaani huku akituma ujumbe wa vitisho kwa binti
wa miaka 16 anayedaiwa kumbaka.
Kutokana
na mfululizo wa habari hiyo ambayo imekuwa ikichapishwa na gazeti hili,
Profesa Kapuya kupitia kwa wakili wake Yasin Memba, ametishia
kuliburuza mahakamani endapo halitamwomba msamaha ndani ya siku saba.
Mbali na kutishia kulipeleka Tanzania
daima na baadhi ya mitandao ya kijamii mahakamani, pia Profesa Kapuya
alikana kumfahamu binti anayedai alibakwa huku akikanusha kumiliki simu
namba 0784993930 ambayo imekuwa ikitumiwa kuwasiliana naye ikiwemo
kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (sms) wa vitisho.
No comments:
Post a Comment