TTCL

EQUITY

Sunday, March 10, 2013

MUME WA MTU SUMU...

Jamani msione watu wanaishi nyumba nzuri asubuhi kila mmoja anatoka na gari lake kwenda ofisini yanayoendelea humo ndani ni KUTA ndio zinayazuia.Jana lilitokea bonge moja la fumanizi hapa jijini Dar.......likikuwa kama ifuatavyo.


Mama aliyefumania akisimulia kwa jazba vile ilivyokuwa...anasema yeye na mumewe walikuwa na ugomvi na kawaida wakigombana yeye hurudi kwao kupumzika.Sasa ugomvi ulipotokea yeye akahamia chumba cha watoto akawa amelala kimyaa.Kumbe usiku mumewe karudi na mwanamke mwingine akaingia nae ndani kama kawa na aliporudi mkewe aliwaona ila akaamua kukaa kimyaa akasubiri kukuche.Kulipokucha jana asubuhi mama akahakikisha watoto wameenda shule ndio akaanzisha fumanizi.......
 
Huyu ni wifi wa mama mwenye mume akisimulia,wakati haya yakiendelea mume mtu kajifungia ndani kimyaaaaaaaaaaaa!!

Dada akilia kwa uchungu.........jamani kufumaniwa sio mchezo tena kwenye nyumba ya mtu!!!hivi mtu unajiaminije kwenda kwenye nyumba ya mtu anayoishi na mkewe na watoto,ni hamu au kutokuwa na akili???? Dada anasema mwanaume alimwambia mkewe ayupo kasafiri ndio akaingia ndani kujivinjari.Na yeye na huyo muwe wa mtu ni wapenzi wa muda mrefu tu.

Bidada akapigishwa saini aandike kwa maandishi kuwa kafumaniwa wapi kwa nani na aahidi hatarudia tena kwenda nyumba za watu.

Nguo ya ndani ikaokotwa......hawa wanawake wambea kinasa cha mwenzenu mwakibeba bila wasiwasi hahahahahahahahah

Dada akapigwa sachi

Akakutwa na hirizi tatu...na inasemekana siku hizi wanawake wengi wanaotembea na waume za watu wanaloga sana na huyu mama anasema mara nyingi wakigombana na mume wake anamwambia mke wangu nisaidie mie sijielewi kama nachanganyikiwa.....

Mama mzazi wa dada mwenye nyumba ndio alikuja kutuliza hili fumanizi kwa kumsihi mwanae ayaache yapite na asipigane amuache tu mgoni wake aende salama...haya mama beba vitu vyako uende.

Dada akitoka taratibu kwa aibu.
Hili ni fumaninizi la watu fulani waliokatika ndoa na wana watoto watatu lakini sisi wengine tunajifunza nini katika hili???Mie ninayo mengi sana ya kusema ila nakuachia wewe.

No comments:

Post a Comment