TTCL

EQUITY

Sunday, March 10, 2013

HERI YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Mwanamke ni dada,shangazi,mama,bibi,mama mdogo,mama mkubwa,mke na mpenzi.Siku hii ya wanawake duniani tuisherehekee tukionyeshana upendo na mshikamano.Wanawake sisi wenyewe ndio tunaangushana wenyewe kwa wenyewe.Mwanamke akilianza jambo kama hajafanikiwa basi wanawake wenzie wataanza kumtia moyo na kumwambia atafika tu.Akishaanza kuonyesha mafanikio mwanamke huyo huyo ataibua vikwazo,maneno,kejeli na kila karaha za kumshusha mwanamke mwenzie.Na hili ndio adui yetu mkubwa tunapigana vita sisi kwa sisi.Tutafikaje?
 Mimi binafsi mpaka kufika hapa nimekutana na vikwazo vingi lakini nimepambana.Japo inafika wakati watu wanakuona mbaya ila lazima uwe na maamuzi hata yale yaliyo magumu.Mwanamke ukijitoa sana,ukiwa muelewa sana,ukiwa mpole sana wapo wanaokuchukulia kama dhaifu na kuona ni haki yao wewe kujitoa kwao lamiza tuwe na mipaka.Mimi naamini mwanamke UKIJIAMINI na ukiwa na IMANI utafanikisha lolote lile duniani.Mimi ni mkristu hata bwana Yesu alisema ukiwa na IMANI utaweza kuamuru mlima usogee na ukasogea.Na hili litawezekana kama ukijiamini na ukiwa na imani.Ukijiamini utatambua nguvu yako,sauti yako,uwezo wako wa kufanya lolote.Ukijiamini utajipenda na utaweza kuwapenda wengine.Ukijiamini utaweza kusimamia ndoto yako na kuakikisha unaifanyia kazi ili kuwa kweli.Ujijiamini hutanyanyasika wala kuwa jalala la wengine kutupa uchafu wao.
 Tunasafari ndefu sana lakini kwa imani tutafika tuendelee kuwa imara,shupavu,tusimamie mipaka yetu,tusimamie ndoto na malengo yetu,tusikatishwe tamaa na yoyote kubwa zaidi TUJIAMINI.

No comments:

Post a Comment