TTCL

EQUITY

Sunday, March 10, 2013

JINSI YA KUISHI NA WATU WENYE TABIA NGUMU (HOW TO DEAL WITH DIFFICULT PEOPLE) (Jielewe wewe na uwaelewe wengine pia)







4. Unafanya nini unapopingwa? (what do you do when you are critized)
Wako watu wanaopendelea kupinga wengine katika kila kitu, hata katika vile visivyostahili kupingwa,hakuna chochote chema kinachoweza kusemwa na yeyote, bali yeye peke yake. Hata kama kilichosemwa kina ukweli kwa asilimia kubwa basi mtu huyu atajitahidi walau kurekebisha hata lugha tu, ili mradi kisipite hivihivi bila yeye kukipinga japo kidogo (hawa ndio wale wenye tabia ngumu). Hali hii huwapa kufurahi na kujijengea nguvu kwa jinsi wanavyopinga wengine. Ni kweli upinzani mwingine ni wa ukweli na unajenga lakini hapa nakazia wale wanaopinga ili tu kujifurahisha nafsi zao na kuwafanya wale wanaowapinga waumie mioyo. Je unapopigwa, unajibuje? Je unajitetea au unajishusha na kukubali kila kinachopingwa kwa kuamini kuona anayepinga yuko sawa na kwa hiyo unayameza maoni yako yote, bila kuchambua kwa kina mapingamizi hayo. Kunajinsi ambavyo unaweza kumkabili au kumjibu anayekupinga na ikawa kama umeweka petroli kwenye moto, upinzani utawaka na hata kuleta magovi, lakini pia aiko njia ambayo unaweza kumjibu mtu huyu na ukanyamazisha fukuto lote.

5. Je unamtazamo hasi (mtazamo usiofaa) na wa kudumu katika kitu fulani? Mfano; Labda  unasema “mambo yangu hayaendelei tangu nihamie katika nyumba hii au “Mambo yangu yanakwama tangu nimuoe au niolewe na huyu” “Ni matatizo tu tangu tuoane” “Watoto hawa hasara tu.” n.k. Mtazamo huu hasi, waweza kukugharimu sio tu kukunyima raha bali pia waweza kuharibu hisia zako na za wengine pia. Ukijikuta katika hali hii ni vema kujifahamu na kujitahidi kuelewa nini tatizo husika na jitahidi kubadilisha mtazamo wako. Tafuta vile vitu ambavyo unaweza kuvitazam katika mtazamo chanya hata kama ni vidogo. Tafuta kuviongelea vile unavyovipenda zaidi ya vile usivyovipenda.
 

6. Je unazimeza hisia zako zote, zilizo nzuri na zilizo mbaya? Je unaona ni ngumu sana kusema “nakupenda” “umependeza” “umeniudhi” n.k. labda unaweza kusema neno moja  tu na siyo lingine. Wengi wetu tumekuzwa katika mazingira ambayo tunahofu kusema chochote ili tu tusije tukamkwaza mtu, hata kama tunaumizwa au tunajisikia vema kusema kitu fulani, lakini tunajizuia. Na badala yake tunakwenda kusemea pembeni. Yamkini kunyamza kunaweza kuwa kwa faida katika baadhi ya mazingira lakini sio hata katika kukubali vitu visivyofaa. Hakuna ubaya wowote katika kuelezea jinsi unavyojisikia moyoni mwako ili mradi tu unaeeleza kila unachokihisi kwa hali njema na sio kwa hasira au shari. Katika hali hii kamwe hutowapoteza marafiki zako, na kama kuna yoyote aliye rafiki atasumbuliwa na hili basi usihofu, kubali tu kumpoteza kwa kuwa hakuwa wa muhimu au wa msaada sana kwako.

Hali ya kujifanya hujaumia au hujakwazika na wakati umekwazika na unalia ndani kwa ndani inaumiza na kufanya ujisikie vibaya sana. Inakufanya uzidishe mazingira ya msongo wa mawazo (stress) hasa pale unapojiwazia wewe mwenyewe zaidi ya kushuhulika na wale waliokuudhi. Mtazamo wako jinsi unavyojiona wewe mwenyewe huathirika sana, na pia waweza kujisababishia tatizo hasa pale wale wenye tabia ngumu watakapo kugundua kuwa huwezi kusema chochote hata ukiumizwa na hii itawafanya wakugeuze mpira wa kuchezea.


7. Je Wewe ni kati ya wale wanaojiamini kusema chochote wanachokifikiri bila kujali matokeo yake? Hembu fikiri jinsi unavyojisikia pale ambapo mtu au watu wengine wangefanya hivyo hivyo kwako. Je unataka kuwasababishia wengine maumivu ya moyoni? Kusema chochote kinachoshuka toka kichwani mwako kupitia kinywani mwako bila kufikiri juu ya matokeo au athari zake kwa wale wanaokusilikza au waliokuzunguka kwaweza kukupotezea marafiki na kuishusha hadhi yako kwa urahisi sana. Mara nyingi mtu wa jinsi hii huweza kujikuta akiwa pweke na anayepingana na ulimwengu (kila mtu anamchukia), hii ni kati ya hisia za kuhuzunisha na kuumiza sana muda wote, lakini pia huumiza zaidi pale unapogungua kuwa ni maumivu uliyojitakia mwenyewe. Peke yako unajikuta umetegwa na mtego wa kihisia na kukuzamisha usipoweza kujikwamua tena.
  na mtaalamu wetu wa saikolojia Bw. Chris Mauki

No comments:

Post a Comment