TTCL

EQUITY

Friday, March 27, 2015

SERIKALI YAWATOLEA UVIVU WACHIMBAJI WADOGO

Serikali wilayani Kahama imetoa siku 14 kwa wachimbaji wadogo wa dhahabu wa mwabomba kutoka kwenye eneo la makazi yaliyomo ndani ya leseni ya mwekezaji na badala yake wahamie eneo la kijiji cha Mwabomba kilichopo kwenye kata ya Idahina

Agizo hilo limetolewa na mkuuwa wilaya ya Kahama benson Mpesya baada ya wachimbaji hao kufikia makubaliano kati yao na wizara ya madini ambayo ni kugawana maeneo ya kufanyia uchimbaji na mwekezaji huyo anayefanya utafiti kwenye eneo hilo

Katika agizo hilo Mpesya amesema tayari wizara ya madini imetoa leseni nne ndani ya eneo hilo la mwekezaji wa kampuni ya Carton Miyabi Tanzania Limited ambalo wachimbaji hao wataendelea kuchimba huku wakiishi nje ya eneo hilo.

MKUU WA WILAYA YA KAHAMA BENSON MPESYA.

Awali kamishina wa madini Tanzania Paul Masanja katika barua yake ameeleza kuwa ndani ya eneo la mwekezaji huyo limetobolewa sehemu nne za namba moja namba mbili darafuma na namba sita ambapo tayari wizara yake  imetoa leseni katika maeneo hayo yatakayomilikiwa na wachimbaji

Hata hivyo masanja ameeleza kuwa pamoja na kulitoboa eneo hilo mwekezaji huyo amepewa masharti ya kutangaza kuanza kwa mgodi ifikapo mwaka 2016 na kama atashindwa eneo hilo atataifishwa na kupewa wamiliki wengine

Kufuatia hali hiyo serikali wilayani Kahama imewataka wachimbaji hao wanaoishi kwenye eneo la mwekezaji huyo wahame ili wampishe aendelee na shughuli zake na wao waendelee kuchimba kwenye maeneo waliyotengewa kwa kuwa kuhama kwao hakutaathiri shughuli za uchimbaji kutokana na maeneo wanayoishi siyo ya uchimbaji.

No comments:

Post a Comment