TTCL

EQUITY

Thursday, February 9, 2017

Makonda Aitwa Bungeni Kujieleza Kwa Madai ya Kutoa Kauli za Dharau Dhidi ya Bunge

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kauli moja limewaita mbele ya Kamati yake ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na DC wa Arumeru Alexander Mnyeti kwa madai ya kudharau Bunge.
 
Maamuzi hayo ni sehemu ya maazimio manne ya  Bunge yaliyopishwa usiku huu dhidi ya viongo wanaoteuliwa na Rais hasa wakuu wa mikoa na wilaya, ambapo azimio lingine ni kumtaka Waziri wa TAMISEMI kutoa maelekezo kwa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kutoingilia majukumu yasiyo yao.
Hatua hiyo inafuatia hoja iliyotolewa bungeni hapo na Mbunge wa Ukonga, Mwita Waitara, kufuatia kauli inayodaiwa kutolewa na Mkuu wa Mkoa wa  Dar es Salaam Paul Makonda inayodaiwa kuwa ni dharau kwa Bunge.
Pia Mwita amedai kuwa viongozi mbalimbali hasa wakuu wa mikoa na wkuu wa wilaya wamekuwa wakitumia madaraka yao vibaya kiasi cha kuingilia majukumu yasiyo yao, na wakati mwingine kuingilia majukumu ya Bunge, na kutolea mfano Paul Makonda na Mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha, Alexander Mnyeti.
Baada ya hoja yake kukubaliwa na Mwenyekiti wa kikao hicho Mh Andrew Chenge, wabunge wameijadili ambapo wabunge kadhaa akiwemo Ester Bulaya, Zitto Kabwe, Saed Kubenea na Joseph Musukuma wamepata fursa ya kuchangia ambapo kwa kiasi kikubwa wote wameoneshwa kukerwa na  kauli hiyo inayodaiwa kutolewa na Paul Makonda, pamoja na utaratibu wa wabunge kukamatwa bila utaratibu.
Wakati mbunge Zitto Kabwe akipendekeza kuitwa mbele ya kamati viongozi waliotuhumiwa, Ester Bulaya amepasua jipu kwa kusoma ujumbe wa vitisho aliodai umetoka kwa kiongozi mmoja aliyeteuliwa na Rais.
Akichangia mjadala huo, Waziri anayehusika na Bunge pamoja na sera Mh. Jenista Mhagama amewataka wabunge kutomuhusisha Rais Magufuli na makosa yanayofanywa na viongozi aliowateua ambapo amesema kuwa kwa mujibu wa sheria Rais ana majukumu yake, na wakuu wa mikoa na wilaya wana wajibu wao, hivyo kama kuna RC au DC anakwenda kinyume na sheria au kuingilia Bunge, anapaswa kuwajibishwa mwenye.
Baada ya mjadala huo, Chenge amewahoji wabunge wanaokubaliana na mapendekezo ya mtoa hoja, ambapo wabunge wote wameitikia kuunga mkono mapendekezo hayo manne na kuwa maazimio rasmi ya Bunge.

Mwanasheria wa CHADEMA na Mbunge wa Singida MAshariki amefikishwa Mahakamani.


  ​

DAR: Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na mashtaka manne ya uchochezi.
Wakili wa Serikali Kishenyi Mutalemwa  aliwasilisha maombi ya kupinga dhamana yaTundu Lissu kwa madai kwamba   amekuwa na mwenendo unaohatarisha amani si tu kwa wanajamii, bali hata kwake mwenyewe kwa kuendelea kutoa maneno ya uchochezi. Hakimu Huruma Shaidi, ametupilia mbali ombi hilo la serikali na kumpa  Tundu Lissu dhamana ya sh. Milioni 20

---- Update: 1
Image may contain: 1 person, smiling, sittingSerikali imeleta hati ya kiapo ambayo inazuia Mh. Tundu Lissu asipewe dhamana.
Kibatala ambaye ni Wakili wa mtuhumiwa amepinga kuwa hicho kiapo kilicholetwa hakina mantiki yoyote kisheria kwa sababu kimeletwa kwa kuvizivizia. Halafu kina makosa mengi, kinazungumzia kuhusu kesi nyingine ambazo amewahi kutuhumiwa nazo, ambazo hazina uhusuiano na kesi ya leo. Kiapo hakitaji kimewahi kutolewa mbele ya Mwanasheria gani, kimepigwa muhuri tu.
Kibatala amelalamika kwamba uwepo wa kesi zingine hata kama zingekuwa mia moja (100) bado haziwezi kuzuia mtuhumiwa kupewa dhamana.
Kiapo kilichotolewa na serikali hakionyeshi ni katika Sheria ipi ambazo zinahusiana na hii kesi ili huyu mtuhumiwa asipewe dhamana.
Wamezungumzia kwamba mtuhumiwa asipewe dhamana kwa sababu ya usalama wake lakini wakashindwa kueleza tangu mwezi wa Januari 2017 alipofanya kosa analotuhumiwa, muda ambao sasa mwezi mzima alikuwa anaishije na labda kama amewahi kutoa taarifa kituo chochote cha Polisi au kwenye vyombo vyovyote vya dola kuwa anatishiwa usalama wake izingatiwe pia Lissu ni Mbunge. Hawajaeleza popote kwamba usalama wa Lissu unatishiwa kwa namna gani mathalani amewahi kukosowa na risasi wapi na wapi.
Wakili Kisenyi (tumefanikiwa kupatikana jina moja kwa sasa) ambaye ni mmoja wa jopo la Mawakili wa Serikali linaloundwa na Mawakili wane (4), ameomba dakika 20 ili akapitie vitabu vya Sheria kuangalia makosa yaliyotajwa kuwemo kwenye kiapo chake.
Hakimu amekataa na kuwaeleza Mawakili wa Serikali kuwa ndiyo maana mlikuja wanne na kuongeza kuwa pamoja na kwamba mliwapatia wenzenu kiapo hapa hapa lakini wao wamejibu kwa hoja nyingi.
Hakimu ameonekana kutokuwa mnyonge na kutoa dakika 10 tu.
Kesi itaendelea baada ya muda huo ili hakimu atolee maamuzi na ifahamike kama Lissu atapewa dhamana au lah!
Related image
-----Update: 2
Wakili wa Serikali, ndugu Kisenyi amekuja kujibu hoja zilizowasilishwa na upande wa utetezi kuhusu hati ya kiapo.
Wakili Kisenyi anasema Mahakama isiangalie makosa yaliyopo katika hati ya kiapo iliyowasilishwa na Mawakili wa Serikali.
Anasema mahakama ijiridhishe na mhuri uliopo kwenye kiapo na isihangaike kuangalia kiliapwa kwenye ofisi gani maana mhuri unaonyesha umegongwa na Wakili aliyopo Dar es Salaam.
Na kuhusu hoja kwamba hakuna facts zinazonyesha kuwa Askari anayemtuhumu Mh. Lissu amepata wapi habari za mtuhumiwa, Wakili Kisenyi amejibu kwamba Askari amezipata kwa njia za Kiintelijensia kwa kuwa yeye Mpelelezi.
Juu ya hoja ya usalama wa mtuhumiwa, Mawakili wa Serikali wamesema kuwa si lazima uwe usalama mtuhumiwa mwenyewe maana maneno anayoweza kutoa akiwa nje ya mahakama au Polisi yanaweza kusababisha uvunjivu wa Amani kwenye jumuiya nzima na jamii nzima ikahathirika hata kama si yeye pekee.
Kwa hiyo wameweka msisitizo kuwa kiapo kipo sawa.
Baada ya kuwasilisha majibu ya hoja, Mawakili wa Serikali wameiomba Mahakama ikubaliane na hati ya kiapo na hivyo imnyime Mh. Lissu dhamana.
Kesi imeharishwa tena kwa nusu saa. Hakimu atarejea baada ya muda huo kuja kutoa huku

-----Update: 3
Dhamana ya Mh. Tundu Lissu ipo wazi!
Maamuzi juu ya hukumu kama yalivyotolewa na Hakimu.
    L1.jpeg
  • Vifungu vyote vilivyotumiwa na Mawakili wa Serikali kuzuia dhamana havikukidhi mahitaji ya kisheria na hivyo si miongoni mwa sababu zinazoweza kuzuia dhamana
  • Kuhusu masuala ya usalama wa mtuhumiwa, Hakimu kasema hakuna taarifa zozote za kina zilizotajwa kwenye kiapo kuthibitisha kuwa mtuhumiwa au jamii inaweza kuhatarika
  • Kiapo kilichowasilishwa na upande wa Serikali kimekuwa na mapungufu mengi, kimekosesewakosewa kimaandishi na hakikuwa na namba ya kesi wala hakikuonyesha kimechukiliwa wapi
  • Kufuatia maelezo hayo, Hakimu amehitimisha kwa kusema Mh. Tundu Lissu anaruhusiwa kudhaminiwa.
  • Patrick J. Assenga amejitokeza kumdhamini kwa dhamana ya TZS 20,000,000/= (milioni ishirini).
  • Kesi itaendelea tena tarehe 06/03/2017
  • Hali nje ya mahakama ilikuwa ya ulinzi mkali. Askari wenye silaha walikuwa wametanda. Haikuweza kufahamika haraka walikuwa na lengo gani. Lakini dalili zilionyesha walitaka Mh. Lissu aingie mikononi mwao akitoka nje ya mahakama. Vijana wa CHADEMA wameweza kuwachezashere askari na kutoweka na Mh. Lissu kuelekea kusiko julikana.
L2.jpeg
Tunaendelea kukuhabarisha kadri matukio yatakavyotokea.



Tuesday, February 7, 2017

'Viroba' kuhamishiwa kwenye chupa


 Image result for viroba
Serikali imesema kama sehemu ya mikakati yake ya kudhibiti unywaji wa pombe maarufu kwa jina la 'viroba' itawaagiza wafanyabiashara wanaohusika kuzihamishia pombe hizo kwenye chupa kubwa ili vijjana wanaozitumia waone aibu kuzibeba kila wakati. 

Akijibu swali la mbunge wa Kigamboni, Dkt. Fautine Ndugulile, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, amesema serikali ilishapiga marufuku biashara hiyo, na sasa kwa mkakati huo utasaidia kuokoa kizazi cha vijana wanaoangamia na kushindwa kufanya kazi kutokana na unywaji wa pombe hizo.
 
Mwijage amesema, pombe hizo zitakapohamishiwa kwenye chupa, gharama yake itakuwa kubwa kiasi cha kuwashinda wanafunzi kununua

Tazama Video......

Wapinzani wamsusia Bunge Naibu Spika

Wabunge wote wa vyama vya upinzani waliokuwa bungeni katika kikao kinachoendelea jioni hii wametoka nje ya Bunge, wakipinga wenzao kufukuzwa bungeni pamoja na kitendo cha Mbunge Tundu Lissu kukamatwa.
Zitto Kabwe akiwa na wabunge wa upinzani mara baada ya wabunge hao kutoka nje ya Bunge
Wabunge waliokuwa wameamuliwa kutoka nje ya ukumbi wa Bunge na Naibu Spika Dkt Tulia Ackson ni pamoja na mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya na Mbunge wa Serengeti Marwa Ryoba.

Wabunge hao watatu wamedaiwa kupinga uamuzi wa Naibu Spika kuhusu muongozo ulioombwa na mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, kuhusu utaratibu uliotumika kumkamata mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mara baada ya Naibu Spika kutoa maamuzi ya kuwaondoa wabunge hao watatu bungeni, ndipo wabunge wengine wa upinzani pia wakaamua kutoka kama ishara ya kupinga maamuzi hayo, pia ikiwa ni ishara ya kupinga utaratibu wa kukamatwa kwa mbunge Tundu Lissu.

Nje ya ukumbi wa Bunge, Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe, amesema wamefikia hatua hiyo kuonesha kuwa uataratibu unaotumiwa kukamata wabunge wakiwa bungeni siyo sahihi, na kwamba kesho wataendelea na vikao vya bunge lakini mapambano yataendelea.

"Kesho tunarudi bungeni, lakini mapambano yataendelea, tunataka kuonesha kuwa utaratibu huu wa kuvizia wabunge kwenye milango ya bunge bila taarifa rasmi ya Spika na bila kuwaeleza wabunge sababu za kukamatwa kwao siyo sawa. Tukilifumbia macho litakuja kumtokea mbunge yoyote hata wa CCM" Amesema Zitto.

Muonekano Mpya wa Mtoto Aliyeokotwa Mtaani Nigeria Akiwa Mwenye Hali Mbaya

Sura ya furaha inaendelea kuonekana kwa mtoto Hope aliyechukuliwa mtaani nchini Nigeria wakati huo akiwa na miaka miwili baada ya kuachwa na Wazazi wake ikisemekana ni Mchawi.

Inasemekana alitelekezwa na familia yake kwa sababu walidhani yeye ni mchawi ambapo baadae akapatikana mtaani na kuchukuliwa na Mwanamke raia wa Denmark Anja Ringgren Loven aliyejitolea kumlea na kuishi nae.

Baada ya kuchukuliwa kutoka mtaani January 2016 picha mbalimbali zimekua zikitoka zikionyesha maendeleo ya Hope akionekana amenawiri kiafya na hata shule anasoma.
Hapa chini ni picha zake za kabla na baada ya kuokotwa…

MWIGULU NCHEMBA ATOA UFAFANUZI WAKUU WA MIKOA NA WILAYA KUSINDIKIZWA NA VING'ORA

WAKUU wa Mikoa na Wilaya ni ruksa kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda kwenye shughuli mbalimbali za utendaji, zikiwamo za ulinzi na usalama katika maeneo yao.
Ufafanuzi huo ulitolewa na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema) aliyetaka kujua kama ni itifaki za kiserikali kwa wakuu wa mikoa na wilaya kutembea na magari ya polisi yenye ving’ora.
Mbowe alishangaa na kuhoji kuwa ni itifaki gani kwa viongozi hao, akatoa mfano wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha kutembea na kikosi cha polisi chenye watu tisa, pikipiki za polisi za kuongoza msafara na gari lenye king’ora.
Waziri Mwigulu alisema, viongozi hao hawaruhusiwi kutembea na misafara yenye magari ya polisi yenye ving’ora wanapokwenda ofisini, labda kama viongozi wa mkoa na polisi wapo ofisi moja, lakini hawakatazwi kwenda navyo wanapoenda eneo la kazi maalumu.
“Viongozi hao wanapokuwa na majukumu ya kwenda kutoa maelekezo au kufanya shughuli zinazohusiana na majukumu ya ulinzi wa maeneo yao, wanaruhiswa kuwa na magari hayo,” alisema.

Msukuma amtaka Paul Makonda aeleze ni wapi anatoa pesa za kwenda kupumzika Paris na Marekani


Vyanzo vya Taarifa katika Kikao cha Bunge kilichoendelea jana jioni, Mbunge wa Geita Ndugu Musukuma amemtuhumu RC Makonda kuwa naye anahusika na dawa za kulevya.

Amedai kawa RC Makonda kwa mshahara wa U RC aeleze ni akina nani walimsafirisha kwenda Marekani na PARIS.

Musukuma ameenda mbele zaidi kasema Makonda aanze na wakwake aliyowapangishia majengo

Tuhuma za Makonda kusafirishwa likizo Nje ya Nchi na kuwa waliomsafirisha wanahusika na madawa ya kulevya hivyo anawalinda inaibua maswali mapya. Je nani anagharimia safari za Makonda Nje ya Nchi.

Hii vita ni kubwa ndugu zangu Tazama Video Hapa Chini ilivyokuwa Bungeni Jana: 

ZITTO KABWE, WABUNGE WA UKAWA NA WABUNGE WA CCM WAINGILIA SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA

Sakata la dawa za kulevya jana lilitikisa Bunge mjini hapa baada ya wabunge kutaka orodha ya ‘wauza unga’ ambayo Rais mstaafu Jakaya Kikwete alisema anayo ili ifanyiwe kazi na mrithi wake, John Magufuli.
Akichangia taarifa za Kamati ya Bunge ya Ukimwi na ile ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alisema Rais Kikwete aliwahi kuutangazia umma kuwa anayo orodha ya vigogo wa dawa za kulevya hivyo alitaka wakamatwe ili watumiaji waachiwe.
“Kikwete alisema anayo orodha ya wauza dawa za kulevya. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mwigulu Nchemba) amfuate kule Msoga ili ampe hiyo orodha. Naamini watumiaji wataachiwa,” alisema.
“Vita ya dawa za kulevya siyo ya Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam), hii ni vita ya Serikali na naamini itamuunga mkono. Mtu akipimwa akionekana ni mtumiaji atusaidie kumpata muuzaji,” alisema.
Mbunge wa Kawe (Chadema), Halima Mdee alimtaka Rais Magufuli kuacha kuendesha nchi kwa sanaa na kutafuta habari zake zipewe uzito katika vyombo vya habari, badala ya kushughulika na tatizo.
Mbunge huyo alisema kwa mwaka 2016/2017, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini ambayo ndiyo yenye dhamana ya vita hiyo haikupata fedha za maendeleo. “Leo bajeti ya tume ni sifuri halafu anasimama mkuu wa nchi anasema vita ipiganwe. Tuache kutafuta vichwa vya habari kwenye vyombo habari,” alisema Mdee.
Aliongeza, “Vita hii inahitaji utashi wa kisiasa. Kikwete alisema anawajua wauza unga kwamba ana orodha. Alipoondoka Ikulu si aliacha mafaili? Orodha unayo hapo Ikulu tusicheze na akili za Watanzania,” alisema.
 
Image may contain: 1 person
 Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe (ACT-Wazalendo) amesema Serikali imeshindwa vita dhidi ya madawa ya kulevya kwa kutokiwezesha chombo kilichoundwa na sheria ili kupambana nayo.“Kamati ya (Bunge) imelalamika kuwa Mamlaka ya Kudhibiti Madawa ya Kulevya ina bajeti finyu na hata hiyo bajeti haitolewi na hivyo kusababisha Mamlaka kukosa vitendea kazi, kushindwa kutoa elimu kwa umma, kushindwa kufanya operesheni za ukamataji wa wafanyabiashara wa dawa za kulevya na kushindwa kutoa ushauri nasaha kwa waathirika,”alisema Zitto.Zitto alikuwa akizungumzia taarifa ya Kamati ya Bunge ya masuala ya Ukimwi imebaini dosari nyingi katika sera ya dawa za kulevya ya mwaka 2004 ambayo imepitwa na wakati.Wakichangia katika taarifa ya shughuli za kamati kwa mwaka 2016/17, wabunge, akiwemo Zitto, walisema dawa za kulevya ni janga la taifa na linahitaji mikakati ya kupambana na siyo kuwaweka rumande waathirika ambao wanahitaji kupatiwa matibabu.Zitto alibainisha kuwa watuhumiwa waliokamatwa katika vita inayoendelea jijini Dar es Salaam wamelazwa ndani kwa zaidi ya siku tatu bila kufikishwa mahakamani.“Baadhi ya watuhumiwa wameelezwa kuteswa na kupigwa na polisi na kulazimishwa kutoa maelezo kwa Polisi," alisema Zitto."Umma haujaelezwa kama watu hawa wamekamatwa na madawa hayo ama wamehisiwa kuwa ni watumiaji tu.”

BAADA YA LIST YA WASANII, LIST YA WABUNGE MADAWA YA KULEVYA KUTAJWA

Kuanzia wiki iliyopita, vita dhidi ya Madawa ya kulevya iliyoibuliwa na mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, inazidi kuchukua sura mpya kila kukicha huku wengine wakitega masikio kwenye vyombo vya habari kutaka kujua kitu gani kinaendelea huko Mahakamani.
 Bunge
Vita hiyo juu ya madawa ya kulevya imefika mpaka bungeni na baadhi ya wabunge walikuwa wakitoa hoja mbalimbali huko mjini Dodoma.

Mbunge wa Ulanga, Goodluck Mlinga jana alisema yeye yupo tayari kuwataja baadhi ya wabunge wanaohusika na biashara hiyo.

Mbunge huyo awali alizungumzia mambo mbalimbali yakiwemo masuala ya elimu lakini la mwisho aliweza kuzungumzia suala hilo ambalo kwa sasa kila mtu anataka kutambua nini kinaendelea.

Goodluck Mlinga
"Suala ninalotaka ni hili suala linashika headline ni suala la madawa ya kulevya, naomba niwaambie sisi viongozi naomba niquote, ‘nitasema ukweli uongo kwangu mwiko.’ Kwahiyo nitakachotaka kukisema mtu yeyote akitaka anihukumu akihukumu chama changu kwanza, na kama wewe ni mwana CCM utanichukia rudisha kadi ndo unichukie.

"Wafanya biashara wa madawa ya kulevya hakuna asiowajua, tunawajua humu ndani wapo, nje ya bunge wapo, kwanini hatuwataji?" alihoji.

Aliongeza, “Kwanini hatuwataji tunakaa kimya? Mheshimiwa mwenyekiti kama kwa ridhaa yako unaniruhusu mimi nitawataja hata humu ndani. Madawa ya kulevya ni pamoja na bangi, kuna mbunge alisimama humu alisema bangi hazina madhara alijuaje kama hazina madhara kama hatumii? tungeanza na huyu.

"Viongozi wenzangu naomba niwahakikishie kama tutakuwa wanafiki mbinguni sisi ndiyo tutakaokuwa kuni, tutakuwa kuni mbinguni tunawafumbia macho watumiaji wa madawa ya kulevya tunakula nao.

"Nimpongeze ndugu yangu Paul Makonda kwa kuthubutu kutaja neno madawa ya kulevya lakini nimhakikishie kila marafiki watano wanaomzunguka watatu ni wafanyabiashara wa madawa ya kulevya, aanze na hao.”

TUNDU LISSU NA SAKATA LA KUSHIKILIWA NA POLISI...!!

Image may contain: one or more people and people standing
 Mbunge wa Singida mashariki nchini Tanzania Tundu Lissu 
 
Kiranja wa bunge upande wa upinzani na mbunge wa Singida mashariki Tundu Lissu alikamatwa siku ya Jumatatu nje ya bunge na kusafirishwa hadi Dar es Salaam kujibu madai yasiojulikana
Kwa mujibu wa gazeti la The Citizen nchini humo, kiongozi wa upinzani Freeman Mbowe {HaiChadema} aliwaambia waandishi kwamba bado hawajajua sababu za kukamatwa kwake.
''Ni kweli alikamatwa na amesafirishwa hadi Dar Es Salaam. Tayari tumewasiliana na wakili wetu na analifuatilia swala hilo''.
Kulingana na Gazeti hilo kamanda wa polisi mjini Dodoma Lazaro Mambosasa alithibitisha kukamatwa kwa kiongozi huyo na kusema kuwa wamepokea agizo kutoka Dar es Salaam, ''tumemkamata kwa uhalifu aliotekeleza na maandalizi ya kumsafirisha yanaendelea'',alisema katika simu.
Aidha gazeti hilo limemnukuu dereva wa Bw Lissu, Simon Makira akisema mwajiri wake alikamatwa mwendo wa saa kumi na moja jioni alipokuwa akitoka katika eneo la bunge ,''alipokuwa akitoka bungeni alifuatwa na maafisa wa polisi waliokuwa wamevalia nguo za kawaida waliosema wamekuja kumkamata''.
''Aliwauliza kwa nini walitaka kumkamata na iwapo walikuwa na kibali.Hakuonyesha chochote isipokuwa vitambulisho vyao na wakamwambia anatakiwa kuwasilishwa mahakamni siku ya Jumanne''.
''Baadaye alipekwa hadi ndani ya gari'' na kuondoka.

SAKATA LA MADAWA YA KULEVYA LAENDELEA KUCHUKUA SURA MPYA BUNGENI

Kufuatia Sakata la dawa za kulevya kuendelea kurindima nchini na Mkuu Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akiongoza katika vita hivi, jana mjini Dodoma Bungeni, wabunge wanataka orodha ya ‘wauza unga’ ambayo Rais mstaafu Jakaya Kikwete aliwahi kusema anayo ili ifanyiwe kazi na Rais wa sasa Dkt John Magufuli.
Halima Mdee, Mbunge wa Kawe (Chadema), alimtaka Rais Magufuli kuacha kuendesha nchi kwa sanaa na kutafuta habari zake zipewe uzito katika vyombo vya habari, badala ya kushughulikia tatizo.
Aliongeza kuwa mwaka 2016/2017, Tume ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini ambayo ndiyo yenye dhamana ya vita hiyo haikupata fedha za maendeleo. “Leo bajeti ya tume ni sifuri halafu anasimama mkuu wa nchi anasema vita ipiganwe. Tuache kutafuta vichwa vya habari kwenye vyombo habari,” alisema Mdee.
Pia aliongeza, “Vita hii inahitaji utashi wa kisiasa. Kikwete alisema anawajua wauza unga kwamba ana orodha. Alipoondoka Ikulu si aliacha mafaili? Orodha unayo hapo Ikulu tusicheze na akili za Watanzania,” alisema.
Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe alisema Rais Kikwete aliwahi kuutangaza wazi wazi kuwa anayo orodha ya vigogo wa dawa za kulevya hivyo alitaka wakamatwe ili watumiaji waachiwe. “Kikwete alisema anayo orodha ya wauza dawa za kulevya. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi (Mwigulu Nchemba) amfuate kule Msoga ili ampe hiyo orodha. Naamini watumiaji wataachiwa,” alisema. “Vita ya dawa za kulevya siyo ya Paul Makonda (Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam), hii ni vita ya Serikali na naamini itamuunga mkono. Mtu akipimwa akionekana ni mtumiaji atusaidie kumpata muuzaji,” Bashe alisema.

UPDATE TAARIFA KUTOKA MAHAKAMANI


Takriban watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu asubuhi hii.
Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani hadi hivi sasa ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Petit Man, Tunda (model wa kike) na wengineo.

 Image may contain: 4 people, people sitting
 Image may contain: 2 people, outdoorImage may contain: one or more people, people sitting and indoor

Fahamu Sababu za U.T.I kuwapata Wajawazito


Dk. Marise anapatikana Marise Dispensary, njia panda ya Mabibo mkabala na kituo cha mafuta. Simu: 0713 252 394au tutembelee katika ukurasa wetu wa facebook Sweetness of afenction
Na Dk. Marise Richard WAPO wanawake wengi wanataka kujua sababu za wengi wao kuugua ugonjwa wa U.T.I (Urinary Tract Infection). Wengine wamekuwa wakidhani kwamba tatizo la kutokwa na uchafu ukeni ni ugonjwa, wazo hilo si sawa kwani huo ni ugonjwa tofauti kabisa na U.T.I
Tunapozungumzia maambukizi katika njia ya mkojo yaani U.T.I, inamaanisha ni kutoka eneo la nje ya utupu hadi kwenye kibofu na kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo. Kama maambukizi yako katika eneo la kutoka kwenye kibofu hadi kwenye figo, kitaalamu huitwa Lower Urinary Tract Infection na yakihusisha eneo la juu ya kibofu jina hubadilika na kuitwa, Upper Urinary Tract Infection.
Maambukizi katika njia ya mkojo au kama unavyojulikana kwa wengi U.T.I huathiri mfumo wa mkojo ikiwa ni pamoja na ureter ambayo ni kama bomba linalosafirisha mkojo kutoka kwenye figo, pia kibofu cha mkojo na mrija wa kutolea mkojo nje yaani urethra.
Ugonjwa huu unaathiri zaidi kibofu cha mkojo na urethra lakini unaweza pia kuathiri figo. Maambukizi haya yakiathiri sehemu za chini za kibofu cha mkojo kitaalamu huitwa Simple Cystitis au Bladder Infection, na maambukizi hayo yakitokea sehemu za juu za mfumo wa mkojo huitwa Pylonephritis au Kidney Infection.
Ugonjwa huu husababishwa na bakteria anayeitwa Escherichia Coli (E. Coli) na tatizo hili husababishwa kwa kiasi kikubwa na bakteria ambao makazi yao ya kawaida ni kwenye utumbo mpana, hivyo huwa wanapatikana pia kwenye haja kubwa.
Lakini baadhi ya watu wanaweza kupata tatizo hili kutokana na kuingiwa na fangasi ingawa pia zipo sababu nyingine chache. Bakteria wa Escherichia Coli hawasababishi peke yao U.T.I bali huambatana na wengine waitwao Staphylococcus, Saprophyti cus, Pseudom onas, Enterobacter na kadhalika. Maambukizi katika njia ya mkojo lazima yawe ni kwenye njia ya mkojo na si pengine popote.
SABABU ZA U.T.I KWA WANAWAKE Mara nyingi maambukizi haya kwa wanawake husababishwa na kutojisafisha vizuri sehemu za siri na kuvaa nguo za ndani zilizochafu. Pia huweza kusababishwa na matumizi ya pedi za kike zenye kemikali ya kukata harufu ambazo huua bakteria wa asili wa eneo la uke na kuwapa fursa bakteria wanaosababisha maradhi haya kuzaliana kwa wingi.
Halikadhalika upungufu wa homoni ya wanawake iitwayo Oestrogen husababisha bakteria wanaosababisha maambukizi katika njia ya mkojo kuzaliana kirahisi. Matumizi ya baadhi ya dawa kwa muda mrefu, unywaji wa vinywaji vyenye sukari kwa muda mrefu na kutokunywa maji ya kutosha pia huchangia tatizo hili.
Uwepo wa mawe katika figo na mirija ya figo pia ni mojawapo ya chanzo cha maambukizi haya katika njia ya mkojo. Sababu nyingine inayosababisha U.T.I ni matumizi ya maji machafu wakati wa kujisafisha au kuoga ambayo huweza kuweka bakteria kwa urahisi na kusababisha mwanamke kupata ugonjwa huo. Uchafu wa vyoo ni sababu nyingine, kwani matumizi ya vyoo ambavyo ni vichafu huweza kusababisha mwanamke kupata U.T.I kwa sababu ndani ya choo kuna bakteria wengi ambao wanaweza kusababisha ugonjwa huo.
Matatizo haya ya maambukizi licha ya kuwapata zaidi wanawake, huwakumba pia watoto wadogo wa kike kutokana na sababu za kimaumbile ambapo viungo vyao vya uzazi, njia ya mkojo na haja kubwa vipo jirani. Watoto wa kiume ambao hawajatahiriwa nao huweza kupata maambukizi rahisi ya U.T.I iwapo watajisafisha kwa kutumia maji yasiyo salama ambapo huwa rahisi kwa bakteria kubaki katika ngozi inayoning’inia (govi).
Pia wanaume watu wazima ambao hawajatahiriwa wanaweza kupata maambuzi ya U.T.I kutokana na sababu tuliyoitaja ambapo pia ni rahisi kwao kuambukizwa Ukimwi kama watafanya ngono zembe na ndiyo maana tohara kwa wanaume husisitizwa. Maambukizi yanayoshambulia mfumo wa mkojo husababishwa zaidi na bakteria wanaoishi katika mfumo wa haja kubwa kwa kuingia na kujikita katika mfumo wa mkojo. Bakteria wengine wanaoleta maambukizi katika njia ya mkojo ni wale watokanao na magonjwa ya zinaa kama kisonono, klamidia, trimonas na fangasi ambapo huwaathiri watu pale wanapojamiiana bila kutumia kinga na watu wenye maradhi hayo.
Ili kuepuka kupata maambukizi katika njia ya mkojo, mara kwa mara, ni vyema kutumia kinga na kwa wanawake wanashauri kila wanapomaliza kufanya tendo la ndoa wakojoe ili kuondoa bakteria walioingia au waliokaa katika tundu la mkojo wakisubiri kuingia.

Monday, February 6, 2017

Ukiyataka mafanikio yoyote makubwa na ya muda mrefu kuwa kiziwi msikivu!

Successful businesspeople raising hands upward.Ni muda mwingine tulivu kabisa tunakutana kupitia safu hii nikiamini kwamba umzima na unaendelea kupambana kuhakikisha maisha yako yanakuwa mazuri.

Mimi namshukuru Mungu kwa kuwa amenipa afya njema na maarifa ambayo nayatumia katika kuyaboresha maisha yangu lakini pia kuboresha maisha yako kwa kukuandikia makala ambazo naamini zinaweza kuyabadili maisha yako endapo utazifanyia kazi.
Mpenzi msomaji wangu, katika kipindi chote ambacho nimekuwa nikizungumzia kuhusu masuala ya mafanikio, nimekuwa nikisema kwamba unaowaona leo wana mafanikio, walipambana na hawakukata tamaa pale walipokumbana na changamoto mbalimbali.
Hawa ni wale ambao walijua fika kwamba kukata tamaa ni adui mkubwa wa mafanikio. Unapojaribu jambo mara moja ukashindwa kisha ukakata tamaa, ni dhahiri hukuwa umedhamiria kusaka mafanikio.
Wenye dhamira ya dhati huwa hawakati tamaa, watajaribu tena na tena na tena mpaka pale ambapo wataona ndoto zao zimetimia. Na wewe unayesoma makala haya unatakiwa kuwa hivyo.
Lakini, tambua wapo baadhi ya watu wanaokuzunguka ambao watafurahi kukuona unaendelea kuishi maisha duni. Wanakuwa na ile dhana kwamba ukifanikiwa utaringa, hutawaheshimu lakini pia utaonekana uko juu yao.
Kutokana na hilo usishangae watu hao wakakupiga vita na wakati mwingine kukukatisha tamaa kwenye yale unayoyafanya. Watakuambia huwezi kufanikiwa kwa sababu elimu yako ni ndogo au watakuambia huwezi kupata mafanikio kwa kuwa uko kijijini.
Watakuaminisha kwamba bila kuwa na elimu kubwa, bila kwenda mjini huwezi kufanikiwa. Ukiwa na akili ndogo zisizojua kuchambua mambo, unaweza kuona wanachokisema ni kweli na ukajikuta unapunguza kama siyo kuacha kabisa jitihada za kupambana kutafuta mafanikio.
Ndiyo maana nikasema kwamba, wewe kama wewe unatakiwa kujiaminisha kwamba unaweza kuwa kama hao unaowaona wana mafanikio makubwa. Jiambie kabisa kwamba kukata tamaa kwako ni mwiko.
Ukiwa na mawazo hayo, wale waliojikatia tamaa ya maisha hawawezi  kukushawishi muwe kwenye mkumbo mmoja. Lazima utakaa mbali nao na kutafuta wale ambao unaamini wanaweza kuwa na mawazo kama yako.
Nilishawahi kusema kwamba, ukiwa ni mtu wa kutaka mafanikio, marafiki zako wawe na mawazo hayo. Kaa mbali na watu wanaokuambia maneno ya kukukatisha tamaa, fahamu hao ni adui wengine katika kufanikiwa kwako.
Kwa maana hiyo usikubali wale waliokata tamaa wakukatishe tamaa, pambana huku ukijua kwamba hakuna wa kuyabadilisha maisha yako isipokuwa wewe mwenyewe.
Ukikubali ndani ya nafsi yako kwamba umeshindwa na huwezi kufanikiwa, hakuna muujiza utakaojitokeza. Utaendelea kuogelea kwenye dimbwi la umasikini mpaka pale utakapoamua kubadili fikra zako.
Hivyo basi, dawa ya wale wasiopenda mafanikio yako ni kukaa nao mbali na kukubali uwezo ulionao bila kufikiria watu wanasema nini juu yako. Amini unaweza, kubali changamoto na uzifanyie kazi kisha muombe Mungu akuongoze katika kila unalolitenda.
Kwa leo naomba niishie hapo ila nikuambie tu kwamba kama una lolote ambalo linakukosesha amani, usikae nalo likazidi kukuumiza, unaweza kuwasiliana na mimi kupitia namba za simu zilizopo hapo juu ili niweze kukushauri.