MBUNGE mteule wa Mikumi kupita Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema), Joseph Haule aka Profesa Jay, amemtaka Rais John
Magufuli kumteua msanii mmoja kuwa mbunge katika nafasi zake 10, ili
akawakilishe kundi wasanii bungeni.
Profesa Jay, ambaye pia ni msanii wa muziki wa
kizazi kipya, amesema kuwa Rais anapaswa kufanya hayo kwa vile serikali
ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), imewatumia wasanii hao katika harakati
zake za kuingia madarakani.
Akizunguza na wandishi wa habari nje ya viwanja vya Bunge mjini hapa
jana, Profesa Jay, amesema kuwa Rais anapaswa kutambua umuhimu wa
wasanii hao badala ya kuwatumia katika mambo mbalimbali ya kisiasa kisha
kuwatelekeza.
“Wanasiasa wamekuwa wakiwatumia sana wasanii wakati wa kampeni lakini wakimaliza wasanii husahaulika kabisa,” amesema Prof. Jay.
Akizungumzia mpasuko kati ya wasanii ambao walikuwa wakishabikia
chama tawala na kuchukia vyama pinzani, amesema hana kinyongo nao kwani
kila mtu alikuwa na mapenzi yake lakini anashukuru kuwa wako
waliyomuunga mkono japo walikuwa wakishabikia CCM, ambapo aliwatajana
majina kuwa ni Mwinjuma Hamisi (Mwana F), na Judith Wambura (Lady Jay
Dee).
Prof. Jay, amesema wapo baadhi ya wasanii ambao walidhani kuwa
kuingia bungeni ni jambo ambalo haliwezekani kwa msanii hususani kupitia
katika chama cha upinzani.
“Mimi nimewasamehe wasanii wote jambo hawakuwa katika upande wake
lakini pia nawapongeza wale wote ambao walikuwa na mimi cha msingi sasa
tuungane na tufanye kazi,” amesema.
Mbali na hilo Prof. Jay amesema licha ya yeye kuwa mbunge wa jimbo la
Mikumi kamwe hawezi kuachana na fani yake ya mziki kwa kuwa fani hiyo
ni sehemu ya mafundisho kwa jamii.
Kuhusu kuchaguliwa kwake kuwa mbunge Prof. Jay amesema yeye ni mbunge
wa jimbo ambapo anatakiwa kuwatumikia wananchi wote bila kujali itikadi
za vyama vya siasa wala dini.
“Kwa sasa ninayo kazi moja ya kuhakikisha ninavunja makundi ninajua
kwa sasa yapo makundi mengi kutokana na uchaguzi lakini jambo pekee ni
kuvunja makundi kwa lengo la kuwapatia maendeleo wananchi,” anasema
Prof. Jay.
Prof. Jay amesema hakuna haja ya makundi hayo kuendelea kuwepo, kwani
kinachotakiwa hivi sasa ni watu Wanamikumi kutumia fulsa zote kwa ajili
ya kujisogezea maendeleo huku wakikumbuka kuwa maendeleo hayana
itikadi.
“Sina sababu ya kuendeleza makundi, wana Mikuni walikuwa kama wakiwa
katika jimbo lao lakini kwa sasa kinachotakiwa ni kuhakikisha wanapata
maendeleo hususani katika sekta ya afya,” alisema Prof. Jay
No comments:
Post a Comment