Serikali imesema kama sehemu
ya mikakati yake ya kudhibiti unywaji wa pombe maarufu kwa jina la
'viroba' itawaagiza wafanyabiashara wanaohusika kuzihamishia pombe hizo
kwenye chupa kubwa ili vijjana wanaozitumia waone aibu kuzibeba kila
wakati.
Akijibu
swali la mbunge wa Kigamboni, Dkt. Fautine Ndugulile, Waziri wa
Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage, amesema serikali
ilishapiga marufuku biashara hiyo, na sasa kwa mkakati huo utasaidia
kuokoa kizazi cha vijana wanaoangamia na kushindwa kufanya kazi kutokana
na unywaji wa pombe hizo.
Mwijage amesema, pombe hizo zitakapohamishiwa kwenye chupa, gharama yake itakuwa kubwa kiasi cha kuwashinda wanafunzi kununua
Tazama Video......
No comments:
Post a Comment