Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa -TAMISEMI Selemani Jaffo amesema serikali imeandaa mpango wa
upatikaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya chini, ili kupunguza
msongamano katika hospitali za rufaa hapa nchini.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, Selemani Jaffo
Jaffo ametoa kauli hiyo bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali
la mbunge wa Segerea, Bona Kalua aliyetaka kujua mpango wa serikali
katika kuboresha upatikanaji wa huduma za afya kwa wakazi wa manispaa ya
Ilala jijini Dar Es Salaam.
Amesema wana mpango wa kuinua hadhi ya baadhi ya zahanati kuwa vituo
vya afya vitakavyokuwa na uwezo wa kutoa huduma zaidi za afya katika
jamii.
Kuhusu tuhuma zinazowakabili askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa
Tanzania – JWTZ, za kuwanyanyasa wavuvi katika maeneo ya Kigamboni na
Kunduchi jijini Dar Es Salaam Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Dkt Hussein Mwinyi ameliambia bunge kwamba taarifa hizo hazijamfikia.
No comments:
Post a Comment