MAAFANDE WAHUSISHWA NA TUKIO LA UTEKAJI WA MWENYEKITI WA JUKWAA LA WAHARIRI, ABSALOM KIBANDA
HII NI KAULI YA ABSALOM KIBANDA
BAADA YA KUTEKWA...............
"Baada ya kutoka kwenye gari, nahisi nilikanyaga sehemu mbaya,
nikateleza na kuanguka wakanifuata...niliona kama watu watatu hivi wakaanza
kunishambulia. Sikuwa nafahamu kilichojiri, lakini nilisikia mwingine akimwambia
mwenzake afande 'mshuti... mshuti' huyo alipoelekeza mtutu na kujaribu 'kushuti'
(kupiga risasi) ilikuwa kama vile imegoma.
“Nikiwa bado niko chini,
wakanipiga kwa kitu cha ncha kali kwenye jicho la kushoto, wakaning’oa meno na
kucha katika vidole vya mkono wa kulia, walinipiga sana na nilipata maumivu
makali. Baada ya kunipiga na kunijeruhi waliniburuza hadi bembeni ya nyumba
yangu na kunitupa na wakaondoka, baadaye majirani na wasamaria wema walikuja
kuniokoa..."
KAULI YA
KAMANDA KOVA...............
Kutekwa kwa Kibanda si
tukio la kihalifu!
Kamanda
wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam,Suleimani Kova, amedai kuwa kutekwa
na kuumizwa vibaya kwa Mwandishi nguli na Mhariri wa New Habari,Absalom Kibanda,
si tukio la kihalifu. Kamanda Kova amedai kuwa tukio hilo limetokana na chuki na
kulipiziana visasi.
Hii ni kwasababu waliomteka na kumshambulia Kibanda
hawakuchukua kitu chochote toka kwake. Alikuwa akizungumza na waandishi wa
habari kutoa taarifa za uchunguzi wa awali wa jeshi la polisi juu ya tukiohilo
lililotokea tarehe 06/03/2013
No comments:
Post a Comment