Askari wa jeshi la polisi Tanzania, Sajenti Patrick Kondwa amejiua kwa kujipiga risasi akiwa katika ofisi yake kwenye ghala lakuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya Mbozi mkoani Mbeya.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya(PICHANI) amekiri kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa chanzo cha kifo hicho bado hakijafahamika na kwamba jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
Sajenti Patrick mwenye umri wamiaka 54 ,akiwa katika ofisi yake kwenye chumba cha kuhifadhia silaha katika kituo cha polisi cha wilaya ya Mbozi amejipiga risasi mdomoni ambayo imetokea kisogoni na kuondoka na uhai wake, tukio ambalo limetokea majira ya saa tisa usiku na kuthibitishwa na kaimu mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya hiyo, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya ileje, Rosemary Staki Senyamule.
Baadhi ya waombolezaji wamesema kuwa wamepokea msiba huo kwa masikitiko makubwa hasa kwa kuzingatia kuwa Sajenti Patrick alikuwani askari mwadilifu na anayeipenda kazi yake.
No comments:
Post a Comment