Kiongozi
wa upinzani aliyetangaza kugombea urais katika Jamhuri ya Kidemokrasi
ya Congo – DRC, Moise Katumbi amekanusha tuhuma za kuwatumia mamluki wa
kukodiwa kuwa walinzi wake.
Moise Katumbi
Katumbi alifika mahakamani jana baada ya kutangaza wiki iliyopita
kuwa atapeperusha bendera ya vyama saba vya upinzani katika uchaguzi wa
rais wa mwezi Novemba nchini DRC.
Polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Katumbi wakati alipofika mahakamani mjini Lubumbashi.
Shirika la Kimataifa la Kutetea Haki za Binadamu limesema tuhuma
dhidi ya mgombea huyo wa upinzani zinaonekana kuchochewa kisiasa.
Rais Joseph Kabila aliyeko madarakani hajatangaza kama atagombea katika uchaguzi huo.
No comments:
Post a Comment