Waziri Mkuu Kassim Majaliwa anatarajiwa kuondoka
nchini leo jioni (Jumanne, Mei 10, 2016) kwenda London, Uingereza
kuhudhuria mkutano wa wakuu wa nchi unaojadili suala la kupambana na
rushwa (Anti-Corruption Summit 2016) utakaofanyika Mei 12.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
Akizungumza
na waandishi wa habari leo mchana, Waziri Mkuu alisema anaenda
kumwakilisha Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli kwa sababu siku
hiyo hiyo, atalazimika kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais wa
Uganda, Mhe. Yoweri Museveni.
“Mheshimiwa Dk. Magufuli ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki
(EAC), na siku hiyo hiyo, mmoja wa marais wa nchi wanachama anaapishwa.
Kwa hiyo amelazimika kwenda kuhudhuria sherehe hizo,” alifafanua Waziri
Mkuu.
Akizungumzia kuhusu mada ya mkutano huo, Waziri Mkuu amesema Tanzania
inafanya vema katika mapambano dhidi ya rushwa na kwamba baadhi ya nchi
zimeanza kuvutiwa na juhudi ambazo Serikali imekuwa ikichukua.
“Waziri Mkuu wa Uingereza ameandaa mkutano huu na alimwalika
Mheshimiwa Rais Magufuli ili ahudhurie akiwa ni miongoni wa wakuu wa
nchi 60 watakaohudhuria mkutano huo. Tanzania ni miongini mwa nchi mbili
kutoka bara la Afrika ambazo zimealikwa kushiriki. Nchi nyingine ya
kutoka Afrika ni Nigeria,” alisema.
Waziri Mkuu atafuatana na Jaji Mkuu wa Tanzania, Othman Chande,
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Kimataifa na Kikanda, Balozi Dk.
Augustine Mahiga, Mkurugenzi wa TAKUKURU, Bw. Valentino Mlowola,
wataalamu wa sekta ya rushwa na wanasheria
No comments:
Post a Comment