Mkurugenzi mtendaji wa Chama cha wanahabari wanawake Tanzania-TAMWA- Valerie Msoka akizungumza na Mwandishi wetu alipomtembelea ofisini kwake. |
CHAMA cha Wanahabari Wanawake (TAMWA) kwa kushirikiana na Ubalozi wa
Canada nchini, leo utafanya mkutano wa siku moja kujadili yaliyojiri
katika kongamano la nchi za Afrika lenye lengo la mpango mkakati
uliojadiliwa kwa ajili ya kutokomeza mimba za utotoni lililofanyika
Desemba, 2015 Lusaka nchini Zambia.
Mkutano huo utakaofanyika katika ofisi za Tamwa Sinza Mori, Dar es
Salaam, utahusisha pia wadau mbalimbali wanaopigania haki za watoto,
kujadili ufanisi na utekelezaji wa sheria zilizopo ili kuweka mpango
mkakati wa kulaani ndoa za umri mdogo Tanzania na jinsi ya kusonga
mbele.
Mkutano huo utajenga imani ya pamoja kutokana na maazimio ya
kongamano la Umoja wa Nchi za Afrika kwa kuwa Tanzania inatambua kuwa
kutokomeza ndoa za utotoni kunahitaji dhamira ya kisiasa, yenye maono na
uwezo wa kuongoza, ushiriki wa wadau mbalimbali, watoto, pamoja na
uwezeshaji katika kupinga mila kandamizi kuanzia ngazi za chini ili
kubadilisha taratibu ambazo husababisha kuongezeka kwa ndoa za umri
mdogo.
No comments:
Post a Comment