Ubalozi
wa India nchini umeingilia kati sakata la kuzuiwa mwili wa Mtanzania,
Abel Machanga aliyekwenda kutibiwa nchini India kabla ya kufariki dunia.
Mwili
wa Machanga umezuiwa katika Hospitali ya Colombia Asia iliyopo kwenye
mji wa Bangarole, hadi deni la dola 16,396 sawa na Sh 35 milioni
litakapolipwa. Ufuatiliaji huo umekuja ikiwa ni siku moja baada ya
gazeti hili kuchapisha habari kuhusiana na kuzuiliwa kwa mwili huo kwa
siku 27 katika hospitali hiyo. Hivi sasa zinafikia siku 30.
Abel
alifariki dunia Desemba 31 mwaka jana baada ya kufanyiwa upasuaji wa
kuondoa uvimbe wa kichwa aliogundulika kuwa nao baada ya kufanyiwa
uchunguzi . Julai mwaka jana, gazeti hili lilichapisha habari ya maradhi
ya kijana Abel hatua iliyosaidia kupatikana kwa dola 7,700 fedha
zilizohitajika kwa ajili ya matibabu yake India.
Kwa
mujibu wa mmoja wa maofisa wa ubalozi, aliliambia gazeti hili kuwa
taarifa hiyo imemfikia, Balozi Sandeep Arya ambaye ametaka kujua ilipo
hospitali hiyo.
Balozi
ameguswa na hiyo taarifa na kama inavyoonekana inaharibu picha ya India
hivyo anataka kuifuatilia hiyo hospitali ingawa sijui ni kwa namna gani
atalishughulikia suala hilo,” alisema
Ofisa
huyo alieleza kuwa hospitali za Colombia Asia ziko nyingi nchini India
hivyo inamlazimu balozi kupata anuani kamili ya eneo ambalo Abel
alipatiwa matibabu na hatimaye kuaga dunia.
Katika
hatua nyingine baba wa Abel, Revocatus Machange amesema mpaka sasa
amepata takribani dola 16,000 ambazo ameshazituma nchini India.
“Namshukuru
Mungu wasamaria wema wamesikia kilio changu nimeshatuma kiasi kikubwa
cha pesa ninachosubiri kwa sasa mwili wake utolewe hospitali”
Kuhusu
gharama za usafirishaji Machanga alisema anasubiri mwili wa Abel
utolewe hospitali kisha masuala ya usafirishaji yatafuata baada ya
kupimwa na kujua itagharimu kiasi gani.
CHANZO ; MWANANCHI.
No comments:
Post a Comment