Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete amesema baadhi ya kauli zinazotolewa na Umoja wa Vyama vya Upinzani (Ukawa), zinaashiria uvunjifu wa amani pindi matokeo ya kura yatakapoainishwa baada ya zoezi la upigaji kura Oktoba 25 mwaka huu.
Rais Kikwete alisema baadhi ya kauli hizo zimekuwa zikionyesha wazi viashiria vya uvunjifu wa amani na upotoshaji kwa kundi kubwa la vijana ambao watakaopiga kura kwa mara ya kwanza.
Akizungumza wakati akizindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao jijini Dar es Salaam Rais Kikwete alisema;
“Wamediriki kusema wazi bila kificho kwamba patakuwa hapatoshi, hizi ni kauli zinazoashiria uvunjifu wa amani. Tunachokisema CCM ushindi kwetu ni lazima na tutashinda kwa kishindo na kwenda nginja nginja mpaka Ikulu.”
Kikwete alisema CCM imejipanga kuhakikisha inapata ushindi katika Uchaguzi Mkuu ujao na kuongeza kuwa ili kufanikisha hilo wamepanga kikosi kazi ambacho kitatembea nyumba kwa nyumba, chumba kwa chumba, mtu kwa mtu ikiwa kwa sasa tayari wameshaanza kufanya kampeni zao kupitia mtandao ya simu za mkononi.
Katika hafla hiyo ya kuzindua kampeni hiyo inayoratibiwa na msanii wa filamu na Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, Rais Kikwete aliwataka wanawake kaungalia mazuri yote yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika kumuinua mwanamke.
Wasanii wa Filamu nchini Wema Sepetu na Steven Nyerere wakimkaribisha Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam kuzindua Kampeni ya Mama Ongea na Mwanao illi aipigie kura CCM.Kampeni hiyo imeratibiwa na Wasanii wa filamu wakuongozwa Wema Sepetu na Steven Nyerere.
Msanii wa Filamu Bi.Wema Sepetu akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalum kwa kutambua mchango wake katika kulinda na kuthamini kazi za wasanii nchini ambapo katika kipindi chake cha uongozi wamepata manufaa makubwa.Wema alikabidhi tuzo hiyo kwa niaba ya baadhi wasanii wa filamu na Muziki nchini wanaoshiriki katika kampeni ya Mama Ongea na Mwanao yenye lengo la kuwahimiza wanawake kuwahimiza watu kuipigia kura CCM kwa kuwachagua wagombea wake katika uchaguzi mkuu mwaka huu.
No comments:
Post a Comment