TTCL

EQUITY

Friday, March 25, 2016

KAMPUNI YA SAMSUNG YAZINDUA SIMU MPYA YA GALAXY S7 NCHINI TANZANIA

ANDREA NGOBOLE


Balozi wa Samsung akimwelezea mteja namna kifaa cha Gear VR kinavyofanya kazi siku ya uzinduzi wa Samsung Galaxy S7 uliofanyika Mliman City mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Mteja akipata maelezo ya Samsung Galaxy S7 kutoka kwa baloz wa Samsung siku ya uzinduzi wa Simu hiyo  uliofanyika Mliman City mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Balozi wa Samsung akipiga selfie na baadhi ya  wateja kwa kutumia Samsung Galaxy S7 siku ya uzinduzi wa Simu hiyo uliofanyika Mliman City mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Mteja akipata maelezo ya Samsung Galaxy S7 kutoka kwa baloz wa Samsung siku ya uzinduzi wa Simu hiyo  uliofanyika Mliman City mwishoni mwa wiki iliyopita.
 
Balozi wa Samsung akimwelezea mteja namna kifaa cha Gear VR kinavyofanya kazi siku ya uzinduzi wa Samsung Galaxy S7 uliofanyika Mliman City mwishoni mwa wiki iliyopita.


Na mwandishi wetu,
Dar-es-Salaam, 19 March 2016: baada ya mchaka mchaka uliokuwa na mafanikio makubwa wa kuweka oda za kununua simu za Samsung Galaxy S7, simu hizi zinazinduliwa rasmi Tanzania tarehe 19 Machi. Kizazi hiki kipya cha Samsung kweye familia ya bidhaa za Galaxy, simu hizi za galaxy S7 na S7 edge zinaongoza kwenye sekta hii kwa kuwa na dizaini nzuri, kamera ya kiwango cha juu, program zenye ubora zilizoungwanishwa na mtandao wa bidhaa na huduma za Galaxy. Hayo yote yatakufanya ufikiri upya uwezo wa simu katika utendaji.

Kiongozi katika uvumbuzi wa simu za mkononi, Samsung imeendelea kuvuka mipaka katika vifaa na huduma, kutengeneza vifaa ambavyo vinasaidia wateja kupata Zaidi katika maisha yao kwa kuzindua kizazi cha saba katika Samsung Galaxy, S7 na S7 Edge kwa watanzania. Uzinduzi rasmi wa Samsung Galaxy S7 na S7 Edge tarehe 19 March umeashiria mwanzo wa kufikiria   namna simu ya mkononi inaweza fanya kazi ambavyo inaeleza tena namna tunavyofikiria kuhusu teknolojia.

Matarajio na furaha ya kuwa wa kwanza kuishika na kumiliki simu mpya ya Samsung Galaxy S7 ilishuhudiwa na namba kubwa ya watu walioweka oda mapema kwa manunuzi yaliyofanyika wiki 2 zilizopita. Simu hizo zilikabihiwa kwa wateja hao waliokuwa wameweka oda mapema. Pia walipewa spika za masikioni zinazotumia Bluetooth ambazo zinajulikana kama Samsung level U.
"Nilisubiria kwa muda mrefu kununua simu mpya na pale Samsung walipozindua simu yao ya Galaxy S7 wiki chache zilizopita, nlijua huu ndio wasaa sahihi. Nilikuwa ni mmoja wa wateja waliojisajili kwa ajili ya oda mapema simu yangu mpya ya Samsung Galaxy S7. Nilipoishika mikononi mwangu nilishtushwa na kasha jinsi walivyokuwa wameifungasha kwa ubora wa juu. Tena, shauku niliyojisikia wakati wa kufungua ina nguvu kama ile ajisikiayo mtu atumiapo bidhaa kwa mara ya kwanza.” Usemi kutoka kwa Mohamed Musa Mteja aliyenunua Samsung Galaxy S7 kwenye duka la Samsung Mlimani City. “ 
Katika Galaxy S7 na Galaxy S7 Edge, Samsung elektronik imezingatia kuacha ukumbusho wa ufunguzi wa simu hiyo. Umakini wa ndani haukuwekwa katika utengenezaji wa simu tu- ufungaji na pakeji pia imefanyiwa mabadiliko” haya yalielezwa na Rayton Kwembe Meneja Bidhaa wa Samsung Elektronik Tanzania, akikaribisha watanzania kushiriki katika uzinduzi.

Uzuri wa simu hii kutoka Samsung ni kuwa inawapa watumiaji hisia nzuri kiganjani mwao lakini ikiwa na kioo kikubwa. Kava lake la mbele na nyuma lina fiti vizuri kiganjani. Ina mwonekano mzuri kuitazama kama ilivyo vizuri katika matumizi. 
Wakati wa uzinduzi wa Samsung Galaxy S7 na S7 Edge, Meneja mkurugenzi wa Samsung Elektronik Tanzania" Thermoforming 3D ni njia mpya ya kipekee katika maendeleo ya teknolojia na kuchangia uvumbuzi na ubunifu kama huo ni muhimu. Hatuna nafasi ya kueleza kikamilifu michakato inayohitajika kuunganisha kioo na chuma , wala hauhitaji kuelewa namna zakiufundi kuelewa ufanisi wa Galaxy S7 Edge mpya. Unachohitaji ni kushika kifaa na kuhisi tofauti katika mikono yako ".

“Wateja waliofanya oda za awali kwa ajili ya Samsung Galaxy S7 na S7 Edge walipewa kipaumbele kwenda kupokea simu zao mapema kabla ya tarehe 19 Machi. Mauzo ya simu hii hapa tanzania yanatarajiwa kuvunja rekodi. Kwa kuongeza samsung imeweka promosheni kwa wateja wote watakao kuwa wananunua simu za samsung galaxy S7 kuanzia siku hii ya uzinduzi watapewa powe bank ya bure kutoka samsung na fursa ya kuingia kwenye droo ya kila siku ya kujishindia samsung Gear VR. Simu hii mpya inakuja na kifurushi kutoka vodacom ya 10 GB na bei yake ni milioni 1.89, Aliongeza Bwana Ibrahim  Kombo Meneja Rejareja Samsung Electronics Tanzania.
Simu za Samsung Galaxy S7 na S7 edge zinapatikana kwenye maduka yote ya Samsung na Vodacom nchi nzima.
Kuhusu Kampuni ya vifaa vya Samsung.
Kampuni ya vifaa vya Samsung ni kiongozi ulimwenguni katika teknolojia, kufungua fursa mpya kwa watu wote kila mahali. Kwa kupitia teknolojia ya hali ya juu na ugunduzi mbalimbali, kampuni ya Samsung inahamasisha ulimwengu na kuleta matumaini ya mabadiliko katika mitazamo na teknolojia zinazolenga katika televisheni, simu, vifaa vya kuvaa, kamera vifaa vya umeme, mtandao, vifaa vya afya na LED. Samsung imeajiri zaidi ya wafanyakazi 319,000 katika nchi 84 na inafanya mauzo ya mwaka dola bilioni 216.7 kujifunza zaidi tembelea www.samsung.com.

No comments:

Post a Comment