Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof JUMANNE
MAGHEMBE,amelitaka shirika la hifadhi za Taifa nchini-TANAPA kuhakikisha
linahifadhi kikamilifu hifadhi zote zilizopo nchini badala ya kutegemea
wafadhili toka nchi rafiki licha ya kuwa baadhi ya hifadhi
zinatambulika kuwa ni urithi wa dunia.
Waziri wa Maliasili na Utalii,Prof Jumanne Maghembe
Waziri MAGHEMBE ametoa agizo hilo wakati akizungumza na Menejimenti
ya shirika la hifadhi za Taifa TANAPA pamoja na viongozi wa vyama vya
mawakala wa utalii jijini ARUSHA,amesema hifadhi zilizopo nchini ndiyo
urithi mkubwa ambao nchi inatakiwa kujivunia hivyo kuna kila sababu ya
kuzilinda.
Pia ameiagiza TANAPA pamoja na hifadhi ya NGORONGORO kuchukua hatua
za haraka kuhakikisha wanafanya mazungumzo na huduma za kibenki ili
watalii wanapokuja nchini wanafanya malipo kwa kutumia mitandao kama
zinavyofanya nchi zilizoendelea.
Mkurugenzi wa Shirika la hifadhi za Taifa –TANAPA-ALAN KIJAZI,amesema
hali ya uhifadhi wa FARU na TEMBO katika hifadhi ni nzuri licha ya
kuwepo kwa changamoto za ujangili.
No comments:
Post a Comment