Serikali imewatoa hofu wananchi kuhusu upatikanaji wa
nishati ya mafuta mara baada ya kuenea uvumi kwenye vyombo vya habari na
kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba hali ya upatikanaji wa
nishati hiyo ni mbaya.
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya udhibiti nishati na maji EWURA, FELIX NGAMLAGOSI
Mkurugenzi mkuu wa Mamlaka ya udhibiti nishati na maji EWURA, FELIX NGAMLAGOSI amesema hayo mara baada ya kurudishwa kwa meli yenye shehena ya mafuta yasiyo na ubora baada ya shirika la viwango na ubora nchini TBS kubaini hilo
Serikali imesema ina akiba ya mafuta ya kutosha katika bohari yake na kubainisha tayari kuna meli inayopakua mafuta bandarini na nyingine yenye shehena ya mafuta iko njiani itawasili wakati wowote
No comments:
Post a Comment