TTCL

EQUITY

Sunday, January 10, 2016

WAZIRI ATAKA KUKAMILISHWA KWA UCHAGUZI WA MEYA WILAYA ZA DSM

Waziri wa nchi Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, GEORGE SIMBACHAWENE amezitaka halmashauri za manispaa ya kinondoni na ilala kukamilisha  uchaguzi wa mameya ifikapo januari 16 mwaka huu.
Waziri wa nchi Tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI, George Simba Chawene

Akizungumza wakati wa kutoa ufafanuza juu ya uchaguzi huo  SIMBACHAWENE amesema zoezi hilo lilicheleweshwa kutokana na dosari ndogo ndogo ikiwa ni pamoja na mvutano wa vyama vya siasa juu ya uhalali wa wajumbe na kutokea mapingamizi ya kisheria mahakamani
Uchaguzi huo wa mameya unaotarajiwa kufanyika hivi karibuni utasaidia manispaa hizo kupata viongozi watakao ongoza kwa kipindi cha miaka MITANO.

No comments:

Post a Comment