TTCL

EQUITY

Tuesday, November 18, 2014

MWANAIKOLOJIA WETU; ZIFAHAMU SABABU ZA KUWASHWA UKENI

Magonjwa ya Zinaa
Kuna aina ya magonjwa ya zinaa ambayo yanaweza kuhusishwa na kuwasha uke. Baadhi ya magonjwa ya zinaa hizi ni Klamidia,  malengelenge sehemu za siri,  na Trichomoniasis. 
Fangasi
Hapa hua na dalili ya kutokwa na ute mweupe na mzito kama maziwa yaliyo ganda(mtindi)
Hedhi
Baadhi ya watu hupata muwasho wakiwa katika hedhi.  Baadhi hali hii hujitokeza wanapokua wamemaliza  kwa sababu estrogen yao hupungua na husababisha kuta za uke kua nyembamba na kavu na kusababisha muwasho. 
 Kemikali
Matumizi ya aina tofauti ya kemikali katika mwili wako, yanaweza kusababisha  muwasho ukeni. Mifano ya  kemikali- ni zenye harufu nzuri, karatasi ya choo,  sabuni za kuogea, kondomu, creams, peds,  mafuta, vitambaa laini , na douches. Jaribu kuondoa/kubadilisha hizi kusaidia kuepuka kero yoyote zaidi.
Baadhi ya magonjwa kama kisukari husababisha muwasho na ingawa hapa dalili za ugonjwa husika pia zitakuwepo, mara chache pia UTI(Urinary Tract Infections) huweza kusababisha muwash.
 
Hizi ni baadhi tu ya sababu, endelea kuwanasi ilikufahamu mengi zaidi.

No comments:

Post a Comment