Washambuliaji wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na polisi
baada ya kufanya shambulio katika hoteli moja maarufu nchini MISRI. Watu
hao walibeba kisu na bunduki na kujeruhi watalii wawili waliokua katika
hoteli hiyo.
Majeruhi wanatibiwa katika hospitali jirani ambapo mmoja wao ana asili ya UJERUMANI na mwingine ni wa DENMARK.
Habari zaidi zinasema kuwa bendera ya kundi la wapiganaji wa ISLAMIC
STATE ilionekana katika eneo la tukio na huenda wauaji hao waliwasili
nchini MISRI kwa njia ya bahari.
No comments:
Post a Comment