Majukumu ya Idara ya Michezo
Mhe. Nape Moses Nnauye Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo |
Idara hii inasimamia na kuratibu shughuli za michezo nchini. Katika kutekeleza majukumu yake, Idara imegawanyika katika sehemu tatu ambazo ni Sehemu ya Maendeleo ya Michezo, Sehemu ya Usajili wa Vilabu na Vyama vya Michezo na Sehemu ya Miundo Mbinu ya Michezo. Majukumu ya Idara hii ni pamoja na;
Kusajili Vilabu na Vyama vya Michezo nchini.
Kushauri na kutoa utaalamu wa utengenezaji wa Miundo Mbinu ya michezo iliyo bora.
Kushauri na kutoa utaalamu wa utengenezaji wa Miundo Mbinu ya michezo iliyo bora.
Kutoa mafunzo ya Uongozi na Utawala pamoja na ufundishaji wa michezo mbalimbali.
Kuratibu ushiriki wa Timu za taifa katika Mashindano mbalimbali ya kimataifa.
Kukuza ushiriki wa Michezo katika taasisi za Elimu, mahali pa kazi na katika jamii kwa ujumla.
Kufanya tafiti za fani mbalimbali za michezo.
Kuendeleza, kufuatilia na kufanya tathmini ya utekelezaji wa Sera, Sheria na mikakati ya maendeleo ya michezo.
No comments:
Post a Comment